Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi katika picha ya pamoja na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akimuelezea jambo Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge
Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge
**********************************
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, ambapo walijadili masuala mbalimbali yanayohusu mahusiano baina ya Tanzania na Italia.

Aidha, walitumia mazungumzo hayo kujadili hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania pamoja na Serikali ya Italia katika kupambana na ugonjwa wa COVID-19.

Mhe. Waziri alifahamisha kuwa hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania kwenye mapambano ya ugonjwa huo zimezingatia mazingiria na hali halisi ya Tanzania pamoja na nchi jirani zinazozunguka Tanzania.

Kwa upande wake Balozi Mengoni alipongeza juhudi hizo za Serikali ambapo alifahamisha kuwa Serikali yake ya Italia inaziunga mkono na kwamba ipo tayari kutoa ushirikiano pale itakapohitajika kufanya hivyo.

Viongozi hao walikubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kihistoria baina ya Mataifa hayo mawili ambao umejikita katika sekta za elimu, afya, utalii pamoja na biashara na uwekezaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...