Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amemuelekeza Mkandarasi wa Ujenzi wa Stand mpya ya mabasi ya Mikoani na nje ya nchi ya Mbezi Louis ambayo ujenzi wake kwa sasa umefikia 70%, kuhakikisha Ujenzi huo unakamilika na kukabidhiwa kwa wakati.

RC Makonda amesema ujenzi wa Stand hiyo unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 50.9 na itakuwa na uwezo wa kuegesha Mabasi Makubwa 700 na Magari Madogo yasiyopungua 300 ambapo ndani yake kutakuwa na Jengo la abiria, Jengo la utawala, Shopping mall's, Hotel, Hostel, kituo cha polisi, matawi ya bank, Migahawa na eneo la wafanyabiashara wa chakula.

Aidha RC Makonda ameelekeza Manispaa ya Ubungo kuhakikisha ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Ubungo unaanza kabla ya Mwezi June na Mkandarasi kuhakikisha ujenzi unakamilika kabla ya Mwezi September mwaka huu kwakuwa tayari Rais Dkt. Magufuli aliagiza kujengwa kwa Hospital hiyo lakini cha kushangaza baadhi ya wizara zimekuwa zikipiga danadana kutoa fedha hizo.

Pamoja na hayo RC Makonda ametembelea Ujenzi wa Jengo la Manispaa ya Ubungo linalogharimu kiasi cha bilioni 6 ambalo ujenzi wake umefikia 65% na kuwataka TBA kuhakikisha Jengo linaanza kutoa huduma kabla ya mwezi August mwaka huu kwakuwa wamekuwa wakisuasua licha ya kuongezewa muda.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...