KAMPUNI ya simu za mkononi ya TECNO imetangaza rasmi kuzindua  simu yake mpya TECNO SPARK 5 yenye kamera tano ambapo uzinduzi huo umefanyika Jijini Dar es Salaam moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii zikiwemo kurasa za mitandao ya kijamii za TECNO.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo meneja mauzo wa TECNO, Mariam Mohamed alisema uzinduzi wa simu hiyo umekuja ukiwa umeambatana na kifurushi cha zawadi kwa wateja yaani (Gift Box) ambayo ni maalum kwaajili ya mteja yeyote anayenunua TECNO SPARK 5.

“Tumekuja na vitu spesho sana kwaajili ya wateja wetu tuna zawadi nyingi sana tofauti tofauti ambazo mteja wetu yeyote  wa TECNO SPARK 5 atakutana nazo na hapa kuna Gift Box na ndani yake kuna vitu tofauti tofauti zikiwemo kibeba funguo(Key holder), selfie stick,chupa, headphone  pamoja na kifuko maalum cha kuhifadhia simu unapokuwa mazoezini” Alisema Mariam.

Meneja mauzo wa TECNO, Mariam Mohamed (Kulia), balozi wa TECNO SPARK 5, Jonijo (Katikati) na Msimamizi wa duka la TECNO, Evelyn (Kushoto). 

Mariam ameongeza kuwa zawadi hizo zitatolewa kwa mteja yeyote atakayenunua TECNO SPARK 5 na kwamba tayari promosheni hiyo imeanza rasmi nchi nzima katika maduka yote ya TECNO.

Wakati wa uzinduzi wa simu hiyo ya TECNO SPARK 5 inayosifika kwa kamera  5 zenye uwezo mkubwa wa kupiga picha mahali popote hata gizani, TECNO pia ilimtambulisha rasmi, Jonijo ambaye ni mtangazaji maarufu wa radio, kuwa balozi wa TECNO SPARK 5.

Kwa upande wake balozi huyo wa TECNO SPARK 5 alisema amekuwa mfuatiliaji mzuri wa matoleo ya TECNO SPARK, kuanzia SPARK 3, SPARK 4 mpaka sasa SPARK 5.

“Mchongo wa TECNO SPARK 5 umekaa poa sana, unajua TECNO sasa hivi wamerahisisha maisha kwasababu  SPARK 5 kuna kioo nimekutana nacho kina maajabu yaani ni inchi 6.6”, SPARK 5 pia ina kamera 5 kwaajili ya picha na video kali wakati wowote” Alisema Jonijo.
                                       Jonijo, balozi wa TECNO SPARK 5.


“Unajua kamera hizi zinavyofanya kazi hata lile tone la maji unaweza kulinasa kwa kamera ya TECNO SPARK 5, na kitu kizuri zaidi betri yake ni 5000mAh hiki kitu ni balaa habari ya kuchaji simu kila siku sahau, hii ukichaji mara moja unakwenda nayo siku 3” Aliongeza Jonijo.

Afisa masoko mitandaoni wa TECNO, Salma Shafii (Kulia) akiwa na Balozi wa TECNO SPARK 5, Jonijo.

Tayari TECNO SPARK 5 ipo kwenye maduka ya simu mikoa yote Tanzania bara na visiwani huku bei yake ikiwa ni rafiki katika kipindi hiki. Kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea kurasa za TECNO za mitandao ya kijamii Facebook, Instagram na Twitter tecnomobiletanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...