Na Khadija Seif, Michuzi tv

SHEIKH Hillal Shaweji maarufu kwa jina la Sheikh Kipozeo amewaomba wazazi na walezi kuwa na hofu ya Mungu kwa lengo la kuimarisha na kuendesha familia zao katika misingi ya kiucha Mungu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Sheikh Kipozeo amesema wazazi na walezi wakiwa na misingi ya dini na hofu ya Mungu familia huwa na amani kubwa n kuishi maisha yenye furaha na kumpendeza Mwenyezi Mungu.

Sheikh Kipoozeo amefafanu wakati nwingine watoto wanakumbwa na mikasa mingi ya malezi kwenye makuzi yao kutokana na kutokuwepo hofu ya Mungu katika familia zao na kusababisha matatizo kila uchao.

"Unakuta baba mlezi anamlawiti mtoto wake bila ya hofu, hilo si jambo zuri katika jamii hata mwenyezi Mungu hapendezwi kabisa,hivyo ili malezi yakamilike lazima pawepo hofu ya Mungu ndani yake. Malezi ya vijana yamekuwa mabaya mno hasa ukizingatia wazazi wengi wanakua na wakati mgumu kuanzia kwenye familia yenyewe kuwa na mpangilio mbaya wa uzazi kila mwaka  ana mtoto.

'Unakuta hawezi kuwaangalia makuzi ya wale watoto wengine kama mwanzo kutokana na kulea mtoto mwengine (Mdogo) na unakuta anasahau wale wengine makuzi yao,"amesema Sheikh Kipozeo.

Aidha, Sheikh Kipozeo amesema suala la unyonyeshaji kwa watoto ni jambo ambalo kila mzazi anatakiwa kulitilia mkazo ili kuhakikisha afya ya mtoto ina imarika siku hadi siku huku akifafanua maziwa ya mama ni kinga ya maradhi. "Hata mimi wazazi wangu  wameninyonyesha miaka mitatu japo miaka miwili ndio sheria kwa mtoto kuwa mwisho wa kunyonya kwake ,"

Hata hivyo Sheikh Kipozeo amewasihi wanaume kutumia njia za uzazi ambazo hazitoleta madhara, kujali familia zao na kuwakinga watoto pamoja na wenza wao na maradhi hasa Ukimwi na Maralia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...