Na Jusline Marco-Longido

Shirika la World Vision Tanzania,Mkoani Arusha limetoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona iliyoenda  sambamba na ulinzi na usalama wa mtoto wa kike katika vijiji 32 Wilayani Longido.

Akizungumza na waandishi wa habari Wilayani humo mratibu wa Kitumbeine DP, Bi.Peruth Daudi alisema kuwa katika suala la uhamasihaji jamii juu ya COVID-19 wameweza kufikia vijiji 19 vilivyomo ndani ya Mradi huo huku vijiji 13 vikiwa nje ya mradi ambavyo  navyo vimeweza kufikiwa elimu hiyo.

Peruth alisema kuwa zoezi la utoaji wa elimu ya mapambano dhidi ya virusi vya corona ni zoezi la wizara ya afya katika uhamasishaji wa ngazi ya kaya katika mikoa iliyoanza kupata maambukizi hayo na ambayo ipo katika hatari ya kuwa na ongezeko la virusi kwa haraka.

Aliongeza kuwa pamoja na utoaji wa elimu hiyo pia suala la ulinzi na usalama wa mtoto wa kike ni jambo ambalo kama shirika wanalipa kipaumbele kwani katika jamii nyingi za wafungaji watoto wakike wapo katika hatari kubwa ya unyantasaji wa kijinsia hasa katika ndoa na mimba za utotoni.

Naye Afisa Ustawi wa jamii Wilaya ya Longido ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Uelimishaji na Uhamasishaji juu ya janga la COVID-19 Bi.Atuganile Chisunga alisema kuwa mbali na utoaji wa elimu ya covid-19,kama wilaya wanaangalia juu ya ulinzi na usalama wa mtoto wa kike na wakiume ambapo wameweza kuifikia jamii hiyo kwa asalimia 70.

Alieleza kuwa katika zoezi la utoaji wa elimu kwenye jamii hiyo waliweza kubaini changamoto ya maji katika vijiji hivyo ambapo kupitia mradi huo wameihamasisha jamii hiyo kutumia vibuyu chirizi kama njia mojawapo ya unawaji wa mikono kwa maji kidogo ambayo itatumiwa na watu wengi zaidi.

Vilevile kamati hiyo iliweza kubaini kuwa mila na desturi za jamii hiyo ya kuozesha watoto wa kike imepata nguvu kufuatia shule nyingi kufungwa na watoto kukaa nyumbani kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Bi.Atuganile aliongeza kuwa jamii nyingi za wafugaji bado zinakabiliwa na changamoto mbalimbali katika suala zima la kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona ambapo kupitia mradi wa Kitumbeine DP wameweza kubaini uvaaji wa barakoa kutumiwa na baadhi ya wanakijiji huku wengine wakishindwa kuvaa barakoa hizo pindi wanapokuwa katika mikusanyiko mikubwa ya watu hivyo elimu ya uvaaji wa barakoa  inahitajika iendelee kutolewa zaidi.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Arusha,Blandina Nkini alisema kuwa kama Mkoa wanashirikiana na wadau mbalimbali na kamati za COVID-19 za halmashauri katika kuhakikisha zoezi la utoaji wa elimu juu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo linafanyika kila ngazi.

Mmoja wa watoa huduma ya afya ngazi ya kijiji aliyejitambulika kwa jina la Thimotheo Lekoja kutoka katika kijiji cha Engushai,kitongoji cha Edonyonajuu, alisema baada ya kupata elimu hiyo kutoka kwa wataamu wa afya aliweza kutembelea kaya zadi ya 82 kuzipatia elimu hiyo na zimekuwa na muitikio mkubwa katika kutekeleza maelekezo waliyoyatoa ya namna ya kujikinga na maambukizi hayo kwa kuweka vibuyu chirizi kwaajili ya kunawa mikono pindi wanapoingia ndani ya boma zao na pindi wanapotoka boma moja kwenda boma nyingine.

Hata hivyo ili kuweza kukabiliana na janga la mlipuko wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya covid-19,mashirika mbalimbali yameombwa kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi hayo katika ngazi za vijijini ambapo ndiko kwenye hatari kuvwa ya kupata maambukizi kutokana na mikusanyiko mikubwa waliyonayo hasa nyakati za miada na masoko.
Janeth Korduni mkazi wa kijiji cha Engushai,kitongoji cha Edonyonajuu, tarafa ya Kitumbeine Wilayani Longido akinawa mikono baada ya kupata elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya COVID-19 waliyopatiwa na Shirika la World Vision Kanda ya Arusha,katika moja ya lango la kuingia kwenye boma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...