Taasisi
isiyo ya kiserekali ya Vijana Think Tank (VTT) @vijanathinktank ambayo
inajumuisha vijana zaidi ya 250, ambayo ilianza kama jukwaa kupitia
group la WhatsApp, siku ya leo wamekabidhi vizimba vitatu vya maji kwa
mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo baada ya kuchangishana pesa kupitia
kundi hilo la WhatsApp na kuamua kupamabana na janga la Corona kwa
kuelekeza nguvu zao kwenye masoko mkoani Dar Es Salaam.
Akiongea
mwakilishi wa taasisi ya Vijana Think Tank (VTT) @vijanathinktank Bi.
Lilian Madeje amesema kuwa waliamua kuchangishana pesa kupitia jukwaa
hilo la WhatsApp ili kusaidia jamii badala ya kujadiliana mambo yao
binafsi kama baadhi ya majukwaa mengine ya WhatsApp yanavyofanya.
Ameongeza
kuwa waliamua kuungana na NVRA ambao pia ndio waliolewa ridhaa ya
kuwakilisha kusimamia ujenzi wa mradi huu, kuanzia kujengwa mpaka leo
umekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo.
Akiongea
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mh. Beatrice Dominic, amewapongeza
vijana hao wa Kitanzania ambao waliona na kuamua kujitoa kwa kuona
umuhimu wa kupambana na janga hili kwa kuchangishana pesa kupitia Group
la WhatsApp, mitandao ya kijamii na hata ana kwa ana.
Mradi
huo ambao umekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo umegharimu
kiasi cha Tsh milioni 3.7 hadi kukamilika ukiwa na vizimba vitatu vya
kunawia mikono kwa kila mtu atakayeingia sokono.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...