SHIRIKA la ndege la Emirates kupitia miradi yao inayotekelezwa kupitia taasisi ya "The Emirates Airline Foundation" imeendelea kugusa jamii zenye uhitaji ambapo katika sekta za elimu, maji na afya huku watanzania wapatao 2912 kutoka maeneo mbalimbali nchini wakiwa wameguswa na mchango wa taasisi hiyo.

Rais wa Shirika la ndege la Emirates na mwenyekiti wa asasi ya Emirates Tim Clark kupitia taarifa iliyotolewa na Shirika hilo ameeleza kuwa Emirates inaangalia njia mbali mbali ya kuchangia katika jamii katika ngazi ya chini hadi ya kimataifa, na wamekuwa wakichangia katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, michezo, utamaduni na wamekuwa wakishirikiana na Serikali, wadau na asasi za kiraia katika kuhakikisha wanawagusa wanajamii walio katika mazingira magumu.

Clark amenukuliwa akieleza kuwa licha ya kuchangia chakula kwa wenye uhitaji asasi hiyo imeenda mbele zaidi na kwa kutoa chakula, mavazi na malazi kwa watoto na hiyo ni pamoja na kuhakikisha wanapata elimu bora ili kuandaa kizazi bora cha baadaye huku ikielezwa kuwa wameendelea kuwashirikisha wateja kote duniani kwa kuwakutanisha na jamii hizo ili waweze kuchangia hata wakiwa mbali.

Mradi wa elimu unaotolewa kupitia shirika hilo umewanufaisha wanafunzi zaidi ya 2670 na walimu 160 na hiyo ni kwa kushirikiana na Warwick Afrika mradi ambao umelenga kuwafundisha wanafunzi wa sekondari masomo ya hesabu na kiingereza na hiyo ni pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu ili kuleta matokea chanya kwa wanafunzi, na ni mpango wa muda mrefu huku ikielezwa kuwa mradi huo wa elimu unaosimamiwa na Emirates tayari umewafikia watu 10,705.

Pia taasisi hiyo imeshiriki katika kutoa mafunzo bure kwa wataalamu 25 wa upasuaji na uokozi na hiyo ni pamoja na gharama za usafiri na katika hilo washiriki waliweza kufanya pasuaji 54 pamoja na kupata mafunzo na mradi huo uliwafikia watu wapatao 76,931.

Kimataifa asasi hiyo ilifanikiwa kuokoa maisha ya watu 90,000 hasa watoto waishio katika mazingira duni..na katika kipindi cha Machi 31, mwaka huu hadi April mosi asasi ilichangia zaidi ya AED 6.5 kwa miradi 22 katika nchi 12.

Asasi hiyo iliyoanza kufanya kazi mwaka 2003 imeshirikiana na asasi zisizo za kiraia katika utekelezaji wa miradi 32 kwa nchi 18 duniani na hiyo ni kupitia michango kutoka kwa wateja.

Imeeleza kuwa kupitia michango iliyotolewa na wateja kutoka sehemu mbalimbali duniani asasi ilitumia milioni 132 katika safari ya asasi 35 kwa mafunzo ya uhandisi na elimu ambapo nchi tano zilizonufaika ikiwa ni pamoja na Bangladesh, Afrika kusini, Uganda na Ghana.

Taasisi ya Emirates Airlines ambayo si ya kibiashara imelenga kuimarisha hali za kimaisha kwa watoto bila kujali itikadi kisiasa wala dini huku mlengo mkubwa ukiwa katika kupambana na magonjwa kwa watoto pamoja na kupunguza vifo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...