Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuujulisha Umma kuwa haihusiki kwa njia moja au nyingine na mashindano ya mbio za Heart Marathon 2020 yaliyokuwa yafanyike tarehe 19 Aprili mwaka huu jijini Dar es Salaam na Zanzibar na kuahirishwa kutokana na kuwepo kwa ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona (COVID – 19).

Mbio hizo za Heart Marathon ambazo zimepangwa kufanyika siku za mbeleni zimeandaliwa na Asasi ya kiraia ya Tanzania Health Summit na siyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Aidha Taasisi inatoa rai kwa wananchi watakaopenda kushiriki katika mashindano hayo kuwasiliana moja kwa moja na waandaaji kama matangazo yao yanavyoonesha.

Hata hivyo kama unapenda kuchangia sehemu ya gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo mdogo kiuchumi wanaotibiwa katika Taasisi yetu unakaribishwa. Unaweza kuchangia kiasi chochote cha fedha kupitia namba ya malipo ya Serikali 994830000022.

Imetolewa na:


Anna Nkinda
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...