Dkt.Tulole Lugendo Bucheyeki mkurugenzi wa kituo cha TARI Uyole akieleza namna walivyojipanga kuhakikisha mkulima anahusika na kilimo bora na chenye tija kupitia Mbegu zinazopatikana katika kituo cha utafiti Uyole.
 Lornad Sabula ni mtafiti kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania kituo cha Uyole,amesema wanashirikiana na mashirika mengine  kama Pata Tija pamoja na halmashauri kikamilifu kwenye kilimo ili kumuwezesha mkulima kunufaika.
 Jafari Mbogela Mkulima wa kijiji cha Ilunda akieleza namna Mbegu bora za Mahindi kutoka Tari Uyule zilivyowasaidia kuinuka katika kilimo.
 Watalamu kutoka kituo cha utafiti TARI Uyole wakiwa katika moja ya shamba la mfano la mkulima wa mahindi kijiji cha Ilunda kata ya Mtwango wilayani Njombe.

Na Amiri kilagalila,Njombe

Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wakulima inayopelekea kukuwa kwa sekta ya kilimo na kusaidia kuongezeka kwa pato la mkulima na Taifa,Kituo cha utafiti wa kilimo (TARI) Uyole,wanasema lengo la kituo kwa sasa ni kuona mkulima Mahiri na anayefanikiwa katika maisha kutokana na kilimo bora na chenye tija.

Amebainisha hilo Dkt.Tulole Lugendo Bucheyeki mkurugenzi wa kituo cha TARI Uyole,wakati akikagua maendeleo ya shamba la mkulima wa Mahindi kupitia mradi wa kuboresha kilimo na maisha ya mkulima kwa kutumia mbegu bora lililopo kijiji cha Ilunda kata ya Mtwango wilayani Njombe.

“Lengo la sasa tunataka mkulima aondoke pale alipo kimaisha,awe mahiri na mkulima huyo tutampima kwa sifa zifuatazo,ambaye atalima kilimo chenye faida,atajitosheleza kwa chakula,ni mkulima ambaye atazalisha mazao kwa ajili ya malighafi ya viwandani,awe ambaye anakuwa na chakula chenye lishe na ambaye hata teteleka na mabadiliko ya hali ya hewa” Dkt.Tulole Lugendo Bucheyeki mkurugenzi wa kituo cha TARI Uyole

Amesema kwa sasa kituo cha Uyole kina aina zaidi ya 8 ya Mahindi zitakazomuwezesha mkulima wa sehemu mbali mbali nchini kufaidika yatakapotunzwa,huku akibainisha kuwa awali walikuwa na mbegu na mbegu kwa ajili Nyanda za juu kusini tofauti na sasa.

“Tuna aina zaidi ya nane ya mbegu za Mahindi ambazo zinaweza zikapandwa sehemu mbali mbali,mwanzoni yalikuwa yanapandwa Nyanda za juu kusini kwa hiyo sasa hivi yanaweza yakpandwa sehemu mbali mbali” Alisema tena Dkt.Tulole Lugendo Bucheyeki mkurugenzi wa kituo cha TARI Uyole

Vile vile amesema kituo kina aina zaidi ya 22 za Maharage huku Soya wakiwa na aina nne.

Lornad Sabula ni mtafiti kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania kituo cha Uyole na meneja wa mradi wa Pata Tija,anasema kwa sasa wanahitaji kubadilisha mtazamo wa kilimo kwa wakulima zaidi ya laki moja katika mazao ya Mahindi,Maharage na Soya.

“Tunataka mkulima wa Soya ajivunie kuwa mkulima lakini pia mkulima wa Maharage ajivunie kuwa mkulima wa Maharage sambamba na mkulima wa mahindi,kwa maana ya sera ya nchi sasa hivi tunaelekea kwenye uchumi wa viwanda,na viwanda vyetu vitatokana na malighafi yanayotokana na kilimo”alisema Lornad Sabula

Jafari Mbogela na Anna Wikichi ni wakulima wa kijiji cha Ilunda wanasema wamepata mafanikio makubwa katika kilimo kutokana na matumizi ya Mbegu bora za kilimo kutoka kituo cha utafiti TARI,hali ambayo imewawezesha kupata zaidi ya gunia 50 za mahindi kwa ekari moja tofauti na awali.

“Kuna mabadiliko makubwa kwenye kilimo kwasababu zamani tulikuwa tunatumia mbegu moja tu ile ya kienyeji sasa walipokuja kutufunza wenzetu hawa wa Uyole ukweli mafanikio yapo maana yake na wenyewe wanakuwa humo humo wanatusaidia cha kufanya”alisema Jafari Mbogela

Mpaka sasa mradi wa kuboresha kilimo na maisha ya wakulima umefanikiwa kuwafika wakulima elfu hamsini wa moja kwa moja katika mikoa ya nyanda za juu kusini,huku wengine wakifikiwa kupitia kwa wagani,maonyesho ya kilimo pamoja vyombo vya habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...