Na Zainab Nyamka-Michuzi TV

TIMU za Ligi Kuu tayari zimesharejea viwanjani kwa ajili ya mazoezi ya pamoja kujiandaa na Ligi Kuu inayotarajiwa kuendelea mapema mwezi Juni mwaka huu baada ya serikali kuruhusu michezo iendelee.

Hata hivyo timu hizo tayari zimechukua tahadhari zinazostahili kupambana na virusi vya Corona kwa kuwapima afya wachezaji wao sambamba na kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.

Kwa upande wa Timu ya Polisi Tanzania, Ofisa Habari wao Frank Lukwaro amesema wamechukua tahadhari kubwa dhidi ya Virusi vya Corona ili kuhakikisha hakuna mchezaji anayepata maambukizi.

Amesema wameanza mazoezi ili kujiaandaa mapema huku wakiendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona na wanaendelea kufuata utaratibu uliowekwa na Wizara ya Afya pamoja na Serikali katika kujilinda na Corona na tumeanza mazoezi mapema ili kujiweka sawa kwa ajili ya kuanza kwa ligi tena.

Aidha, Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema wameweza kuwapima wachezaji wao kabla ya kuanza mazoezi yaliyoanza jana na wamekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa wachezaji wao.

Amesema, walifanya semina na kuwapa elimu wachezaji wao namna ya kujilinda na Corona huku wakiendelea kuchukua tahadhari kujilinda zaidi na hilo ni baada ya kuripoti kambini na kufanyiwa vipimo vya afya.

Mbali na hao, timu zote zimeweza kuwa wachezaji wao wamechukua tahadhari dhidi ya virusi hivyo na wapo makini katika kujilinda na kufanya mazoezi kwa bidii kubwa kwa ajili ya muendelezo wa ligi kuu.

Serikali imetangaza kuanzia Juni Michezo yote irejee baada ya kupungua kwa maambukizi ya virusi vya Corona na itachezwa kwa katika Mkoa wa Dar es salaam katika Viwanja vya Taifa, Uhuru na Chamazi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...