Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Mama Anne Makinda akizindua mpango wa Machinga Afya unaotoa fursa kwa machinga kujiunga na huduma za matibabu kwa gharama nafuu.
Sehemu ya washiriki wa hafla ya uzinduzi wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF.
Mwanachama kupitia mpango wa Machinga Afya akifuarahia baada ya kupokea kadi yake ya matibabu.
Mama Anne Makinda akikabidhi kadi kwa wanachama wapya kupitia mpango wa Machinga Afya.
Mwenyekiti wa Bodi Mama Anne Makinda akishuhudia uwekaji wa Saini wa Mkataba wa Makubaliano ya huduma hiyo kati ya Machinga na NHIF.
Zoezi la utiaji wa saini likiendelea.

Na Mwandishi Wetu


Mwenyekiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mama Anne Makinda amesema umefika wakati kwa Watanzania kuwekakipumbele katika suala la afya kwa kujiunga na mfumo wa bimaya afya unaowahakikishia upatikanaji wa huduma za matibabuwakati wote.


Mama Makinda ameyasema hayo leo (Alhamisi 2Mei,2020wakati akizindua mpango wa Machinga Afya ambaounawalenga wamachinga wote nchini kwa gharama nafuu yashilingi 100,000 kwa mwaka.


Afya ni muhimu kuliko jambo loloteni wakati wa kuwekakipaumbele kwa kuhakikisha tunakuwa na bima ya afya badalaya kuelekeza nguvu nyingi katika kuchangia harusi na sherehezingine ambazo zinahitaji kwanza afya yako iwe njema,” alisema Mama Makinda.


Alisema kuwa tendo la uzinduzi huo ni matokeo chanya ya kazikubwa iliyofanywa na Mfuko kuhakisha kila kundi la wananchilinakuwa na fursa ya kujiunga na huduma za matibabu.

Alisema kuwa kauli ya HAPA KAZI TU iliyotolewa mwaka 2015 na Mheshimiwa Rais DktMagufuli imekuwa na matokeomakubwa sana ambayo kila mmoja kwa sasa anaweza kuyaonakwa macho.


Wakati hii kauli ikitolewa ilikuwa ni ngumu kuielewa lakinikwa sasa unaweza kuielewa kwa kuunganisha matukioyanayoendelea mfano tumeona mambo makubwa ambayo Raiswetu DktMagufuli ameyafanya katika sekta zote na tumeonahata ambavyo amesimama na Watanzania kwenye hiki kipindikigumu cha CORONA hali ambayo imeondoa hofu na watuwameendelea kufanya kazi zao kama kawaida,” alisema.


Alisema kuwa Serikali imefanya kazi kubwa ya uboreshaji wahospitali nchini na huduma za matibabu kwa ujumla hatuainayowezesha upatikanaji wa huduma zote za matibabu kirahisina kuondoa changamoto zilizokuwepo awali zikiwemo zaukosefu wa dawa.


Mfuko umejipanga sana kuwahudumia wananchi na kuwafikiakatika maeneo yaohivyo natoa wito kwa watoa hudumakuhakikisha wanawahudumia wanachama kulingana na maadiliyao ya kazi,” alisema Mama Makinda.

 

 

Naye Mwenyekiti wa Wamachinga Tanzania Bw. Stephen Lusinde akizungumza katika hafla hiyoamesema kwambakitendo cha kuzinduliwa kwa mpango huo ni sawa na Machingakuzaliwa upya wakiwa na matumaini ya ulinzi wa afya zao.


Hakika siku ya leo kwetu ni sawa na kuzaliwa upyahapo awalihatukuwa na uhakika wowote wa ulinzi wa afya zetukupewafursa hii na Mfuko inatuhakikishia usalama zaidi wa mitaji yetulakini uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote,” alisem BwLusinde.


Alitumia fursa hiyo kutoa pongezi zake kwa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa namnaambavyo amehakikisha chini ya uongozi wake kunakuwa nauhakika wa huduma zote za kijamii ikiwemo suala la afyaambalo ni suala nyeti.


Miaka ya nyuma sisi tulijiona kama ni kundi ambalolimetengwa lakini kwa kitendo hiki cha sisi kuanza kutumiahuduma za NHIF sasa tunatembea kifua mbele na katika hilinaomba niwapongeze sana Mfuko kwa kuhakikisha hililinafanikiwa na Wamachinga wote nchini wamepokea hili kwafuraha kubwa,” alisema BwLusinde.


Akielezea namna Mfuko ulivyojipanga kutoa huduma kwakundi hiloMkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Kongaamesema mkakati uliopo ni kutoa huduma bora kwa wanachamana kuendelea kuwafikia wananchi ili waweze kujiunga.


Leo tunaanza na kundi la Wamachinga wa Kariakoo ambaowana utaratibu mzuri sana wa kuratibu wanachama wao nampango huu umelenga kuwawezesha wajasiliamali hawa kwagharama ya shilingi 100,000 tu kwa mwaka hivyoniwahakikishie kuwa upatikanaji wa huduma ni wa uhakikakabisa,” alisema BwKonga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...