Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akizungumza kuhusu malipo ya wakulima wa Kata ya Iglanson kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.
 Afisa Ushirika wa Wilaya ya Ikungi, Gurisha Nsemo akizungumza na Wakulima wa Kata ya Iglanson wakati wa malipo hayo.
 Mkulima, Isack Shango,  akimshukuru Rais Magufuli kwa niaba ya wenzake.
  Mkulima, Magreth Magamba, akizungumza. 

 Wakulima wa Kata ya Iglanson wakisubiri kulipwa. 

  Wakulima wa Kata ya Iglanson wakisubiri kulipwa. 

 Meneja wa Benki ya NMB, Wilaya ya Ikungi, Osward Kayuni, akizungumzia umuhimu wa wakulima hao kufungua akaunti ili malipo yao yalipwe kwa njia ya simu. 
 Choroko zikiwa kwenye mnada.
 Mkulima, Francis Magesa (kushoto) akitafsiri lugha ya kisukuma wakati mama huyo (kulia) alipokuwa akimshukuru Rais Magufuli kwa kuwapelekea mfumo huo.



Na Dotto Mwaibale, Singida

WAKULIMA  Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, wamempongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kuelekeza ununuzi wa mazao yao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.

Pongezi hizo walizitoa mwishoni mwa wiki wakati wa ulipwaji wa fedha zao baada ya kuuza choroko kwa  njia ya stakabadhi ghalani katika Kata ya Iglanson.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akizungumza wakati wa utoaji wa malipo hayo alimshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwajali wakulima.

" Kipekee nimshukuru Rais Magufuli kwa kuelekeza matumizi ya mfumo huu wa stakabadhi ghalani kwani umekuwa ni mkombozi kwa wakulima wetu." alisema Mpogolo.

Alisema katika wilaya hiyo wakulima zaidi ya 500 wamenufaika na mfumo huo ambapo wameweza kupata zaidi ya sh.milioni 139 na kuokoa zaidi ya sh.milioni 54 ambazo wangenyonywa wakulima.

Mpogolo alisema changamoto kubwa iliyokuwepo ni walanguzi hao kujikita kwenye maeneo ya vijiji na kuupinga mfumo huo kwa kuwa ulikuwa ukiwanufaisha kwa miaka mingi.

Alisema wachuuzi walikuwa wanatumia vipimo feki kwani utakuta katika kilo 50 zitazopimwa na mkulima utaona kilo tatu zilikuwa zikikatwa kiujanja na walanguzi hao.  Huku wachuuzi wakinunua kilo moja kati ya sh.400 hadi 600 lakini kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani waliweza kuuza kwa sh.1075 kwa kilo kwenye mnada wa tarehe 14 mwezi Mei 2020.

Mpogolo alitaja changamoto nyingine kuwa ni walanguzi hao kuwalaghai wakulima kuwa vyama vya ushirika vilikiwa havina uwezo wa kuwalipa fedha zao siku hiyo hiyo wakati sio agizo la mfumo.

Akimuongelea mkulima Joyce Nzela ambaye alitoa malalamiko kwa Rais Magufuli wakati alipo simama kwa muda na kuongea na wananchi wakati akiwa njiani kuelekea Dodoma akitokea Chato, ambaye alilalamikia mfumo wa ununuzi wa zao hilo alisema walipofuatilia hakuonekana katika orodha ya wakulima waliopeleka choroko  kwenye AMCOS ya Kijiji cha Mayaha kama alivyodai. Hata hivyo kumbukumbu zilionyesha kwenye mkutano wa kutoa elimu ya mfumo uliofanyika Mei Mosi 2020 Kijiji cha Mtavila kuwa Joyce, alikuwa miongoni mwa wachuuzi walioupinga mfumo na kuwataka wakulima wasiukubali.

" Tulifuatilia tuligundua jina lake halikuwepo kwenye orodha ya wakulima ambao walipaswa kulipwa lakini wenzake, Zuhura na Amina walikuwepo kwenye orodha ya AMCOS ya Iglanson na malipo yao yalikuwepo." alisema Mpogolo.

Mkulima, Isack Shango,  alimshukuru Rais Magufuli kwa niaba ya wenzake na kusema walanguzi walikuwa wakiwanyonya kwa kutumia vyombo vikubwa huku bei ikiwa ndogo.

Alisema walanguzi hao walikuwa wakitumia ndoo maarufu kwa jina la Mozambiki yenye ukubwa wa kuingiza kilo 25 ambayo ikiwa na malighafi walinunua kwa sh.60,00 na bila malighafi walikuwa wakilipia sh.70,000 

Wakulima wengine waliompongeza Rais Magufuli kwa kuwawezesha kulipwa fedha zao kupitia Benki ya NMB ni pamoja na  Magreth Magamba, Emmanuel Ncheyi na Francis Magesa.

Meneja wa Benki ya NMB, Wilaya ya Ikungi, Osward Kayuni aliwataka wakulima hao kufungua akaunti katika benki hiyo ili malipo yao yaweze kufanyika kwa haraka kupitia  simu zao badala ya utaratibu wa kuwapelekea fedha mkononi ambao sio salama.

Wakulima hao wameshukuru mfumo huo kwanza wanapata pesa zaidi  kuliko mwanzo, pili kutumika kwa vipimo vya uhakika na tatu pia kuimarishwa kwa vyama vya ushirika ambapo wamemuomba Rais Magufuli mazao mengine ya mpunga na alizeti yaingizwe kwenye mfumo kwani wananyonywa sana kipindi hichi cha mavuno.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...