Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Chuo kikuu Mzumbe Bi. Rose Joseph akizungumza na Waandishi wa Habari waliofika Chuoni hapo kuona maandalizi ya mapokezi ya Wanafunzi.
Moja ya matanki yaliyosimikwa katika mazingira ya Chuo kikuu Mzumbe kwa ajili ya Wanafunzi kunawa mikono kabla na baada ya kuingia darasani.

Mkuu wa kituo cha Afya Chuo kikuu Mzumbe Dkt.Paschal Songoro akizungumza na Waandishi wa Habari na kuwaonesha maandalizi ya mazingira ya kuwapokea Wahisiwa wa ugonjwa endapo watatokea
Mwanafunzi Hassan Salim akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kupokelewa na kufanya usajili chuoni hapo.
 ***********************************

Wanafunzi waliowasili Chuo Kikuu Mzumbe kuendelea na Muhula wa Pili wa masomo utakao anza tarehe 01 Juni 2020, wameridhishwa na hatua za maandalizi zilizochukuliwa na Chuo hicho kuwakinga na ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya CORONA (COVID- 19).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mahojiano na Waandishi wa Habari waliofika chuoni hapo kukagua maandalizi ya maeneo watakayotumia wanafunzi kusomea, Wanafunzi hao wamesema wamefurahishwa na mazingira waliyoyakuta, na hivyo kuwaondoa hofu waliyokuwa wamejijengea kabla ya kufika chuoni hapo.

“Tahadhari kubwa imechukuliwa, ukifika getini lazima kwanza kupimwa joto la mwili, mbali na uwepo wa vifaa vya kunawa mikono kila sehemu, matangazo ya tahadhari; huku tukisisitizwa kuvaa barakoa muda wote tunapokuwa kwenye mikusanyiko” Alisema Aney Daniel Mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shahada ya Sayansi katika Maendeleo ya Watu.

Awali akizungumza na Waandishi wa Habari waliofika Chuoni hapo kujionea maandalizi ya mapokezi ya Wanafunzi, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Bi. Rose Joseph alisema Chuo kimezingatia miongozo yote iliyotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, kwa kuhakikisha tahadhari zote zinachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuandaa kwa wingi vyombo vya maji tiririka, sabuni, vitakasa mikono, elimu pamoja na kuandaa timu ya wataalamu wa Afya, watakaotoa huduma kwenye Kituo chetu cha Afya.

Baadhi ya wanafunzi wameshawasili chuoni hapo kuanza masomo huku usajili ukiendelea ambapo zaidi ya wanafunzi elfu kumi na moja (11,000) wanatazamiwa kuripoti kwa Kampasi zake zote (Morogoro, Mbeya na Dar-es- salaam).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...