SERIKALI imepongezwa kwa mpango wake wa kujenga vituo vya Afya kila kata,ujenzi wa Hospitali za wilaya na Rufaa hatua inayotajwa imesaidia kuboresha huduma za Afya na kuwepo kwa mazingira ya utoaji huduma bora kwa watumishi wa sekta ya Afya katika mkoa wa Katavi.

Hayo yamesemwa kwa nyakati tofauti na baadhi ya wananchi waliokutwa wakipata matibabu katika Hospitali ya Halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoani Katavi.

Walisema,tangu Serikali ilipoanza ukarabati wa zahanati na ujenzi wa vituo vya Afya na ujenzi wa Hospitali hapa nchini hali ya upatikanaji wa huduma zimekuwa bora na hata watumishi wa sekta ya Afya wanafanya kati zao katika mazingira bora ikilinganisha na siku za nyuma ambako kulikuwa na changamoto kubwa ya mazingira bora ya kazi.

Jackson Lugaraba na mfanyakazi wa Hospiatli hiyo Dkt Rubi Mwita Marwa walisema, wamempongeza sana Rais Dkt John Magufuri kwa kazi mzuri ya kujenga miundombinu ya Afya na kwani imechochea hali ya wananchi kwenda katika vituo vya kutolea huduma pindi wanapoumwa na kuchochea uwajibikaji kwa watumishi wa sekta ya Afya.

Dkt Marwa alisema, ujenzi wa Hospitali ya halmashauri hiyo ambao uko katika hatua za mwishi kukamilika utachochea na kuongeza hamasa kwa wafanyakazi katika suala zima la kutoa huduma mzuri kwa wananchi.

Afisa mipango wa Halmashauri hiyo Pastory Mgaruka alisema,Halmashauri ilipokea shilingi bilioni 1.5 kutoka Serikali kuu na ilianza ujenzi wa Hospitali hiyo katika bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019.


Alisema, kukamilika kwa Hospitali hiyo kutasaidia wakazi takribani laki moja na elfu arobaini wa halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe kuondokana na hadha ya kutembea umbali mrefu hadi Hospitali ya mkoa Mjini Mpanda kufuata baadhi ya huduma muhimu ikiwemo ya upasuaji ambayo haipatikani katika zahanati zilizokuwepo.

Mkaruka alisema, ujenzi huo ulianza kutekelezwa kuanzia mwaka jana kwa gharama ya biliioni 1.5 na mradi huo ni mkubwa na kutakuwa na majengo ishirini na mbili ili kutengeza Hospitali ya wilaya ambapo baadhi ya majengo yamekamilika na kuanza kutoa huduma na majengo mengine yatajengwa kwa awamu na katika bajeti ya mwaka 2019/2020 wametenga milioni mia tano.

Alisema, Hospitali hiyo ni kati ya miradi mikubwa inayojengwa na Serikali katika Halmashauri hiyo ya Mpimbwe ambayo inalenga kusogeza,kuboresha na kuimarisha upatikanaji wa huduma mbalimbali jirani na kuwaondolea usumbufu wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma.

Alitaja miradi mingine iliyotekelezwa na kuanza kutoa huduma ni pamoja na ujenzi wa kituo cha Afya Husevya na Mamba ambayo imekamilika na imeanza kufanya ya kuwahudumia wananchi.

Alisema, Hospitali hiyo ni moja kati ya miradi mikubwa saba inayotekelezwa katika Halmashauri ya Mpimbwe, mingine ni ya sekta ya utawala,maji na elimu ambayo imekamilika na inafanya kazi.

Mganga mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt Edward Sengo amemshukuru Rais Dkt John Magufuri kwa kuleta fedha bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa majengo saba katika Hospitali hiyo.

Alisema, kwa mwaka wa fedha 2020/21 wanategemea kupokea fedha milioni mia tano ambazo zitakwenda kukamilisha ujenzi huo hata hivyo katika Hospitali hiyo wameshaanza kutoa baadhi ya huduma ikiwemo ya wagonjwa wan je(OPD) huduma za mama na mtoto na ushauri nasaha.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Mpimbwe Erasto Kiwale alisema,katika bajeti ya mwaka 2020 wametenga jumla ya shilingi bilioni 1 ambazo zitatumika kujenga nyumba za watumishi ikiwemo ya mkurugenzi na wakuu wa idara.

Aidha amemshukuru Rais Dkt John Maaguri kupeleka fedha katika halmashauri hiyo kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imehamasisha wananchi kufanya kazi za kujiletea maendeleo na kushiriki katika ujenzi wa Taifa kwa njia ya kujitolea.

Alisema, Halmashauri imefanikiwa kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu kwa kujenga vyumba vya madarasa,maktaba,nyumba za walimu,ofisi za serikali za vijiji na kata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...