Na Mwandishi Maalumu
 Balozi wa Tanzania nchini Afrka Kusini Meja Jenerali (Mst) Gaudence Milanzi Jumatatu Mei 25, 2020 amesimamia zoezi la repatriation (usafirishaji) wa dharura) ya  Watanzania pamoja na raia kadhaa wa nchi hiyo waliokwama kutokana na Lockdown na kusitishwa safari za ndege inayoendelea huko, kutoka Johannesburg kuja Dar es salaam.

Taarifa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini humo zinasema kwamba Balozi Milanzi aliratibu na kusimamia zoezi hilo ambapo Watanzania 14 ambao walikwama nchini humo kwa miezi miwili kufuatia Lockdown hiyo.

Raia 12 wa Afrika Kusini pamoja nna raia mmjoa wa Uingereza nao wakajiunga kwenya msafara huo baada ya kuona ni afadhali warejee Tanzania ambako hakuna Lockdown ili kuendelea kufanya kazi kwenye makampuni na taasisi za nchi hiyo.

Akiwasindikiza abiria hao walioondoka kwa ndege ya kukodi ya kampuni ya AS SALAAM AIR ya Zanzibar, Balozi Milanzi aliwapa pole kwa kuwa katika Lockdown ya miezi miwili na kuwatakia safari njema na maisha ya furaha watapowasili Tanzania ambayo ni nchi pekee ambayo imekuwa na msimamo thabiti wa kupambana na gonjwa la COVID 19 lililosababisha nchi zingine kufungia kila mtu ndani.


Hili ni tukio la tatu la repatriation tokea gonjwa hilo liikumbe dunia na kusababisha sintofahamu kila pembe, kufuatia zile safari za India na Falme za Kiarabu ambapo serikali ilituma ndege maalumu kwenda kuchukua wananchi wake waliokwama huko kutokana na Lockdown katika nchi hizo.

Zoezi hilo limekuja wakati Tanzania imefungua rasmi anga lake na kuruhusu utalii pamoja na safari za ndege za kimataifa viendelee kama kawaida, ambapo tayari mamia ya watalii wameendelea kumimimika nchini, huku wengine wakitarajiwa kuwasili kwa wingi baada ya mashirika ya ndege ya kimataifa kuanzisha safari zao.

 
 Sehemu ya abiria Watanzania na wa Afrika Kusini wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O.R. Tambo wakijiandaa kuondoka
 Dawati la ukaguzi wa mwisho wa abiria wanaoondoka katika Uwanja wa O.R. Tambo jijini Johannesburg
Abiria hao wakiwa tayari katika Uwanja wa O.R. Tambo jijini Johannesburg

Upekuzi wa mizigo ya abiria hao katika Uwanja wa O.R. Tambo jijini Johannesburg

Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini a,kiagana na abiria hao katika Uwanja wa O.R. Tambo jijini Johannesburg
Abiria hao katika ukaguzi wa mwisho katika dawati la Uwanja wa O.R. Tambo jijini Johannesburg

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...