Na Mashaka Mhando, Tanga .

WATENGENEZAJI wa vitakasa mikono Jijini Tanga, wametakiwa kuzingatia mahitaji halisi ya utengenezaji wa bidhaa hizo ili ziweze kukabiliana na virusi vya Covid 19.

Akitoa maelekezo hayo kwenye semina iliyoandaliwa na shirika la msaada wa kisheria mkoani hapa la (TAWOREC), Mfamasia wa Jiji Ali Hamza alisema ni lazima vitakasa mikono viwe na vilevi (alcohol) kuanzia wastani wa asilimia 70 ili viweze kuuwa virusi hivyo katika mikono.

"Tunawasihi watengenezaji wa Sanitizer (vitakasa mikono) wafuate taratibu za utengezaji alcohol inatakiwa iwe asilimia 70, hivi ni viwango vipya awali ilikuwa asilimia 60,"alisema.

Mfamasia huyo ambaye pia aliwaelekeza wana-semina ambao ni Wasaidizi wa Kisheria (Paralegal) kutoka halmashauri 11 za mkoa wa Tanga, alisema ipo haja kwa Serikali kuongeza upatikanaji wa malighafi ya kutengeneza bidhaa hizo.

Pia aliwataka watengenezaji wawakilishe bidhaa zao zinapitishwa na mamlaka zinazohusika ili waweze kuzithibisha kwamba zinafaa kwa matumizi yaliyokusudiwa.

Kwa upande wao wasaidizi hao wa kisheria, waliziomba halmashauri zao kuhakikisha wanashirikiana nao katika suala la utengenezaji wa bidhaa hizo ili kuwezesha upatikanaji wake kwa wananchi wengi hasa wa pembezoni mwa mji.

David Sechambo Paralegal kutoka Bumbuli, aliomba halmashauri ziwasaidie waweze kupata malighafi za kutengeneza vitakasa mikono kwa bei itakayokidhi mahitaji yao.

"Tunaziomba halmashauri zetu, kupitia wafamasia, watusaidie hizi Material za kutengeneza Sanitizer kwa bei rahisi, " alisema Sechambo.

Juma Mhina kutoka Paralegal ya Korogwe alitoa Shukrani kwa TAWOREC kwa kuwapatia mafunzo ambayo yamewawezesha kujua kwa undani virusi vya Covid 19 vinavyosabahisha ugonjwa wa Corona duniani.

Dorice Michael wa Paralegal ya Levo Lushoto, amefurahi mafunzo hayo licha ya kuujua ugonjwa wa Corona lakini pia wamefahamu kutengeneza vitakasa mikono.

Awali Meneja wa shirika la TAWOREC, Halima Saguti aliwataka wasaidizi wa msaada wa kisheria, wakafanye kazi zao huku wakichukua tahadhari za ugonjwa huo katika maeneo yao. 
 Mfamasia wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Ali Hamza akiwaelekeza washiriki wa semina hiyo jinsi ya kutengeneza vitakasa mikono
 Baadhi ya Washiriki wa Semina hiyo wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri
 Ofisa Ufuatiliaji na Tathimini wa TAWOREC Charles Lukindo akihamasisha matumizi sahihi ya kuandika taarifa kwa Paralegal hao
Mwanasheria wa TAWOREC Victer Kisaka akiwaeleza namna wanavyotakiwa kutoa msaada wa kisheria katika maeneo yao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...