Baadhi ya picha za wauguzi katika maadhimisho ya Siku ya wauguzi Duniani .

Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya wametoa zawadi  ya Cherehani ikiwa ni kuadhimisha siku ya  wauguzi Duniani.


Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya,  leo wamekabidhi zawadi ya mashine ya cherehani  yenye thamani ya shilingi 1,500,000/= MZRH ikiwa ni mchango wao wa alama ya upendo katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wauguzi duniani.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Mwenyekiti wa  Chama cha Wauguzi(TANNA) tawi la MZRH Bi. Iddah Sewangi amesema mashine hiyo ya kisasa ni sehemu ya kuunga mkono  juhudi zinazofanywa na hospitali katika kuboresha huduma na itasaidia kushona mavazi mbali mbali ya hospitali ikiwemo  ushonaji wa mavazi maalum (PPE) katika mapambano ya janga lilipo sasa la corona.

Akipokea zawadi hiyo kwa niaba ya uongozi wa hospitali, Mkurugenzi Mtendaji   Dkt. Godlove Mbwanji amewashukuru wauguzi hao kwa zawadi hiyo ya mashine ambayo na kusema  imekuja kwa wakati wakati sahihi ambapo sasa kuna kazi ya kuendelea kushona mavazi mbali mbali ya hospitali zikiwemo barakoa.  

“.. Kwa niaba ya viongozi  ninawapongeza kwa  kazi nzuri kubwa na yeye changamoto nyingi ambayo mmekuwa mnaifanya na ninyi kama wawakilishi wa wauguzi wengine walioko kule mawodini, naomba hizi salaam mziifikishe kwao , wauguzi ni jeshi kubwa na tunadhamini sana kazi zenu nzuri kwa ustawi wa hospitali yetu .”

Amesema kuwa katika huduma za matibabu wauguzi ndio wanaokaa na wagonjwa kwa muda mrefu hivyo ni lazima kukutana na changamoto nyingi na kutokana na hilo wameendelea kuonyesha amani  upendo na  ushirikiano kwa kutimiza majukumu yao ya kufanya kazi pamoja.

Leo dunia inasherehekea kumbukizi ya kuzaliwa kwa mwasisi wa wauguzi Florence Nightingale, kwa kuwasha taa ya upendo na kurudia kiapo cha kitaalumakwa  kuendelea kuonyesha njia kwa jamii yenye afya kwa watu wote kizazi cha sasa na kijacho. Pia kutoa elimu, taarifa na huduma bora kwa jamii yote Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wauguzi duniani kwa mwaka huu ni Wauguzi, Sauti inayoongoza Uuguzi kwa dunia yenye Afya.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...