Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, amezitaka  Shule kuacha kutumia ugonjwa wa Covid-19 kama kitega uchumi kwa kuagiza fedha za ziada kutoka kwa wazazi; na kuwa Serikali  itachukua hatua kwa shule zinazofanya hivyo ikiwa ni pamoja na kuzifutia usajili. 

Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo jijini Dodoma alipozungumza na Vyombo vya Habari kuhusu Mwongozo wa Kudhibiti Maambukizi ya Ugonjwa wa Corona (Covid-19) katika Vyuo na Taasisi za Elimu nchini uliotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.

Amesema baadhi ya shule zimekuwa zikitoa maelekezo mbalimbali kwa wanafunzi wakati huu wa kuelekea kufungua shule, ikiwa ni pamoja na kuwaagiza wanafunzi kubeba lita mbili za spiriti, limao za unga na tangawizi, huku wengine wakiweka michango isiyokuwa na uhalali wowote.

“Wanafuzi walikuwa wameshalipa ada kabla ya kufunga shule na walikwenda nyumbani kwa kuwa kulikuwa na changamoto ya mlipuko wa ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona.  Baada ya kazi kubwa ambayo imefanywa na Serikali, hali ya maambukizi imepungua. Ndio maana shule na vyuo vinafunguliwa na wanafunzi wanakwenda kuendelea walipoachia kwa fedha zao walizolipa. Hakuna malipo ya ziada,” amesisitiza Prof. Ndalichako. 

Amezitaka shule kuendelea kuwapa wanafunzi vyakula vinavyowapa vitamin ‘C’ badala ya kuwatuma wanafunzi kuleta vitu ambavyo ni vya kutengenezwa.

Pia amesisitiza shule na vyuo kuzingatia mwongozo wa kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona uliotolewa na  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

“Ni marufuku kwa  wanafunzi kwenda na spiriti shuleni kwani inaweza kuchoma shule na mabweni na pia inaweza kutumika kama kilevi.”
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma( hawapo pichani) wakati akitolea ufafanuzi mwongozo wa udhibiti wa maabukizi ya ugonjwa wa CORONA katika shule na Vyuo na Taasisi za Elimu nchini.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...