Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imemwita Dk. Imni Patterson, Kaimu Balozi wa  Ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa lengo la kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho.

Kaimu Balozi huyo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. 

Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu ameeleza masikitiko yake kutokana na namna ambavyo  Ubalozi huo umekuwa ukitoa taarifa mbalimbali za  ushauri wa kiusafiri  (travel advisory) zinazoandikwa na kusambazwa na Ubalozi wa Marekani kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo suala la namna Tanzania inavyoshughulikia ugonjwa wa COVID-19. 

Akitolea mfano Katibu Mkuu amezitaja taarifa  zilizotolewa na Ubalozi huo siku ya Jumatano  13 Mei, 2020 na ya siku ya Jumatatu  25 Mei, 2020 kwenye mtandao wa “Twitter” wa Ubalozi huo ambazo zote zilionekana kukusudiwa kutoa tahadhari kwa raia wa Marekani waliopo nchini na wanaotarajia kuja Tanzania kuwa jiji la Dar es Salaam siyo salama kutokana na kuwepo idadi kubwa ya wagojwa wa COVID-19.

Tahadhari hizo pia zimeendelea kudai kuwa hospitali nyingi jijini Dar es Salaam (bila ya kuzitaja hospitali hizo) zimefurika wagonjwa wa COVID-19 jambo ambalo siyo kweli na linauwezekano wa kusababisha taharuki kwa Watanzania na wageni kutoka nje ya nchi ilhali hali halisi sivyo ndivyo inavyodaiwa. 

Katibu Mkuu amemjulisha Kaimu Balozi kuhusu umuhimu wa Ubalozi kutoa taarifa zilizothibitishwa hususan kwa sababu serikali haina kizuizi cha aina yoyote kwa Mabalozi kutafuta na kupata taarifa sahihi na zenye ukweli.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu amemshukuru Kaimu Balozi huyo kwa ushirikiano mzuri na wa kihistoria uliopo baina ya Tanzania na Marekani katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, biashara, uwekezaji, ulinzi na usalama na maeneo mengine ya maendeleo.


Emmanuel Buhohela
MKURUGENZI KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI 26 MEI 2020 
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akisalimiana na Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt mni Patterson. Kaimu Balozi huyo ameitwa Wizarani kwa lengo la kutoa ufafanuzi masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho.Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwa katika mazungumzo na Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt mni Patterson. Kaimu Balozi huyo ameitwa Wizarani kwa lengo la kutoa ufafanuzi masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho. Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

 .Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt Imni Patterson akizungumza wakati alipokutana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge. Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akimsikiliza Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini Dkt Imni Patterson. Kaimu Balozi huyo ameitwa Wizarani kwa lengo la kutoa ufafanuzi masuala mbalimbali ambayo Ubalozi huo umekuwa ukiyaandika katika mitandao yake ya kijamii bila ya uthibitisho. Mazungumzo halo yamefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...