Na Editha Karlo,Kigoma.
WATU tisa wamefariki baada ya boti la abiria kuzama katika ziwa Tanganyika, Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi MARTIN OTTIENO amethibitisha.
Kamanda Otieno amesema ajali hiyo imetokea katika eneo la Rasini na kusema kuwa Boti iitwalo "Mv Nzeimana" inalofanya safari zake kati ya Kijiji cha Sibwesa na Ikola limezama ikiwa na abiria 60, ambapo abiria 51 wameokolewa.
Aidha Kamanda OTTIENO amesema chanzo cha ajali hiyo ni upepo mkali uliosababisha boti hilo kukosa muelekeo na hatimaye kupinduka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...