Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Taifa la Israel kwa Tanzania Mhe. Oded Joseph ambaye analiwakilisha Taifa hilo kutokea Nairobi, Kenya.

Kanali Balozi Ibuge katika mazungumzo hayo amweleza Balozi Oded, kuhusu hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kukakabiliana na kusambaa kwa COVID-19 na madhara sambamba na madhara cake.Aidha, pamoja na mambo mengine Wawili hao katika mazungumzo yao wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo ya kuendelea kukuza na kudumisha uhusiano wa kidiplomasia na biashara baina ya Tanzania na Israel.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akifafanua jambo kwa Balozi wa Taifa la Israel nchini Mhe.Balozi Oded wakati wa mazungumzo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiagana na Balozi wa Taifa la Israel nchini Mhe.Balozi Oded mara baada ya kuhitimisha mazungumzo yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...