Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Bujumbura Nchini Burundi kwa ajili ya
kumuwaklilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwenye shughuli ya kuapishwa Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste
Ndayishimiye leo Juni 18,2020. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Burundi
Mhe. Gasten Sindimwa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais Mpya
wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye Ikulu ndogo Gitega Nchini Burundi
alipowasilisha salam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli kwa Rais Ndayishimiye leo Juni 18,2020. kushoto ni
Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya
nne Dkt. Jakaya Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Mpya
wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye Ikulu ndogo Gitega nchini
Burundi leo Juni 18,2020.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Rais mpya wa
Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye wakati Rais Ndayishimiye alipokuwa
akipokea Gwaride la Jeshi la Wananchi wa Burundi baada ya kuapishwa
rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi leo Juni 18,2020 katika
Uwanja wa Igoma Stadium Nchini Burundi. Makamu wa Rais amemuwakilisha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye
Shughuli hiyo.

Makamu wa Rais wa Jarmhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Rais Mpya wa
Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye mara baada ya Rais Ndayishimiye
kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi leo Juni 18,2020
katika Uwanja wa Ingoma Stadium Nchini Burundi Makamu wa Rais
amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli.

Rais Mpya Burundi Mhe. Evariste
Ndayishimiye akikaguwa Gwaride baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri
ya Watu wa Burundi leo Juni 18,2020 katika Uwanja wa Ingoma Nchini
Burundi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Mpya
wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye mara baada ya kuapishwa kuwa
Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi leo Juni 18,2020 katika Uwanja wa
Ingoma Nchini Burundi. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Makamu wa
Rais wa Burundi Mhe. Gasten Sindimwo alipowasili kwenye Uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Bujumbura Nchini Burundi kwa ajili ya kumuwakilisha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye
shughuli ya kuapishwa Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye
leo Juni 18,2020. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...