Ndugu Moses Matiko Misiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime Vijijini, Mkoa wa Mara na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema leo amejivua vyeo vyake vyote ndani ya Chama hicho na kuomba kujiunga na CCM.
Aidha Ndugu Moses Matiko Misiwa ameeleza sababu za kuachana na Chama chake,amesema chama hicho kwa sasa  kimepoteza muelekeo, Hivyo Uongozi wa dhati na wenye matokeo chanya wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk. John Pombe Joseph Magufuli na Uimara wa CCM kwa sasa katika kuwatumikia Watanzania ndio umemkuna zaidi na hatimaye kuchukua uamuzi alioufanya.
Ndugu Matiko amepokelewa na Ndugu Humphrey Polepole na kumhakikishia kuwa amefanya chaguo sahihi kwa wakati sahihi.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...