Mjumbe wa Kamati Kuu na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Munde Tambwe (kulia) akimkabidhi kadi ya CCM, Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Singida, Shabani Limu baada ya kujiunga na chama hicho mwishoni mwa wiki.

Mjumbe wa Kamati Kuu na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Munde Tambwe, akionesha kadi ya Chadema baada ya kukabidhiwa.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Singida, Shabani Limu akila kiapo na wenzake baada ya kujiunga na chama hicho.

Na Dotto Mwaibale, Singida

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Singida,.Shabani Limu amerejea Chama Cha Mapinduzi na kupokelewa kwa shangwe na nderemo..

Limu alipokelewa juzi na kukabidhi kadi ya Chadema kwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Munde Tambwe.

Akizungumza wakati wa hafla ya kumpokea mwanachama huyo mwishoni mwa wiki, Tambwe alimpongeza Limu kwa kurudi nyumbani kujakuongeza nguvu hasa katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.

"Karibu nyumbani tushirikiane kuendelea kukijenga chama chetu cha CCM chama cha wanyonge na kinacho pendwa ndani na nje ya nchi yetu alisema Tambwe.

Limu akizungumza baada ya kurejea CCM alisema ameridhishwa na mwenendo imara wa Chama Cha Mapinduzi katika kushughulika na changamoto za wananchi na yuko tayari kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika kuimarisha kazi anayoifanya Rais Dkt. John Magufuli ya kuwatumikia wanyonge.


" Rais wetu amefanya mambo makubwa katika nchi hii nimeona sina sababu ya kubaki Chadema bali nirudi CCM nyumbani kushirikiana na wanachama wenzangu kwa ajili ya kuchochea zaidi maendeleo ya Mkoa wa Singida" alisema Limu.

Limu alitumia nafasi hiyo kuwasihi wapinzani wengine wanaopenda maendeleo ya nchi yetu kuwa hawana sababu ya kuendelea kubaki huko waliko huku wakinyanyasika na kutengeneza maendeleo ya mtu pasipo maendeleo ya wananchi,,,warejee CCM kuijenga nchi na kuwa sasa Singida imeshaseti mitambo na iko tayari kuingia kwenye uchaguzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...