Na Mwandishi Wetu, Mwanza

WATU wanne wameripotiwa kufariki Dunia na wengine 27 kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakiwa kwenye mtumbwi waliokua wakisafiria katika Ziwa Victoria wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.

Akizungunza leo kuhusu tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Muliro Jumanne amesema lilitokea  Juni 23 mwaka huu ,saa mbili asubuhi katika Kitongoji cha Busele kilichopo Kata ya Bubiko wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.

Kamanda Muliro amesema mtumbwi huo wa abiria unaojulikana kwa jina la One Ten wenye namba za usajili 00238 unaofanya safari zake kati ya  Kome na Bugaza ulipigwa radi na kusababisha vifo vya watu wanne pamoja na majeruhi 27 ambapo kati yao ni wanawake 12 na wanaumme 15.

Amewataja waliofariki Dunia ni Deogratus Mulungu(50), Kumunya andrea(36), ambaye ndio alikuwa Nahodha wa mtumbwi, Simon cherles(36)aliyekuwa Nahodha Msaidizi na  Ndege Abdu(25).

Pia amesema, majeruhi wamefikishwa katika Zahanati ya Kijiji cha Bukiko na wengine Kituo cha Afya cha Bwisya kwa ajili ya matibabu, huku baadhi wametibiwa na kuruhusiwa.

Amesema miili ya marehemu wote imefanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.
 

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...