Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg. John Pombe Joseph Magufuli leo tarehe 01 Juni, 2020 amekagua maandalizi ya kumbi za mikutano na vikao vya chama vinavyotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Ndg. Magufuli akiwa ameongozana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally Kakurwa amekagua kumbi za Kituo cha Mikutano Dodoma (Jakaya Kikwete Hall) ambako utafanyika Mkutano Mkuu wa CCM na pia amekagua jengo la Ofisi za Makao Makuu ya CCM (White House, Jijini Dodoma).

Ndg. Magufuli amewapongeza wajumbe wa Sekretarieti ya CCM na wasimamizi wa ukarabati uliofanyika katika majengo hayo ya CCM ambayo yanatarajiwa kuwa tayari ifikapo tarehe 20 Juni, 2020.

Ndg. Magufuli amesisitiza kuwa pamoja na kufanyika kwa mchakato wa uchaguzi ndani ya chama, Uchaguzi Mkuu lazima utakuwepo na hivyo amewataka wanachama wote wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kujitathmini na kujiridhisha kama wanatosha kugombea nafasi wanazoomba.

Ameonya kuwa kuelekea katika mchakato huo wanachama hawana budi kuweka mbele maslahi ya chama badala ya maslahi yao binafsi na pia kutofanya vitendo vya kuwagombanisha na fujo ambavyo vitakavyokiumiza chama.

“Chama chetu kinayo demokrasia ya kutosha, lakini demokrasia hii ndani ya chama isije ikatumika kuleta fujo, kutugombanisha na kukiumiza chama, tuweke maslahi ya chama mbele na tutumie nafasi hii kukiimarisha chama chetu” amesema Ndg. Magufuli.

Ndg. Magufuli amewataka wana CCM kote nchini kutembea kifua mbele na kuyasema mambo yote ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa wananchi, badala ya kuacha jukumu hilo kwa viongozi wachache.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa mara baada ya kukagua kazi za ukarabati wa ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma leo tarehe 1 Juni 2020.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula kuhusu Maendeleo ya ukarabati wa ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention jijini Dodoma leo tarehe 1 Juni 2020.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa pamoja na Makamu Mwenyekiti CCM- Bara Philip Mangula akikagua kazi ya ukarabati wa maeneo mbalimbali ya ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention jijini Dodoma leo tarehe 1 Juni 2020.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akipita kukagua ukarabati wa Ukumbi NEC katika Makao Makuu ya CCM White House mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akipita kukagua ukarabati wa Ukumbi NEC katika Makao Makuu ya CCM White House mkoani Dodoma.



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na baadhi ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi CCM katika Makao Makuu ya CCM White House Dodoma leo tarehe 1 Juni 2020.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...