Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Joseph Pombe Magufuli amewapandisha vyeo Maafisa Wakuu kuwa Brigedia Jenerali na wengine kuwa Meja Jenerali kuanzia tarehe 02 Juni, 2020.



       Miongoni mwa waliopandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali ni pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kanali (Balozi) Wilbert Augustin Ibuge na Kamishna wa Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Kanali Francis Ronald Mbindi. 

Waliopandishwa cheo kuwa Meja Jenerali ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Charles Mang’era Mbuge, Kamishna Jenerali wa Magereza Brigedia Jenerali Suleiman Mungiya Mzee, Mkurugenzi Mtendaji wa MSD Brigedia Jenerali Gabriel Saul Mhidze na Mkuu wa Chuo cha Maafisa Monduli Brigedia Jenerali Ibrahim Michael Mhona.

        

Imetolewa na

Luteni Kanali Gaudentius G. Ilonda

Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano

+255754-635-412

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...