Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (katikati) akisisitiza jambo kwa
wasanii wa Sanaa ya uchoraji maarufu Tingatinga (hawapo pichani) wakati
alipowatembelea kuona shughuli zao na kusikiliza changamoto mbalimbali
wanazokabiliana nazo mapema hii leo 24 Juni 2020 jijini Dar es Salaam,
kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw.
Godfrey Mngereza na kulia ni Afisa Utamaduni toka wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Habibu Msami.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akisisitiza akifafanua jambo kwa
wasanii wa Sanaa ya uchoraji wakati alipowatembelea kuona shughuli zao
na kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo mapema hii leo
24 Juni 2020 jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wasanii wa sanaa ya
uchoraji wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Juliana Shonza (hayupo pichani) Wakati Naibu Waziri huyo
alipowatembelea kuona shughuli zao na kusikiliza changamoto mbalimbali
wanazokabiliana nazo mapema hii leo 24 Juni 2020 jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (katikati) akiangalia kazi ya uchoraji
ikiendelea wakati Naibu Waziri huyo alipowatembelea wasanii wa Sanaa ya
uchoraji maarufu Tingatinga kuona shughuli zao na kusikiliza changamoto
mbalimbali wanazokabiliana nazo mapema hii leo 24 Juni 2020 jijini Dar
es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha
Ushirika cha Tingatinga Bi. Zena Salum akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia) Wakati
Naibu Waziri huyo alipowatembelea kuona shughuli zao na kusikiliza
changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo mapema hii leo 24 Juni 2020
jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia) akiangalia kazi mbalimbali za
uchoraji wakati Naibu Waziri huyo alipowatembelea wasanii wa Sanaa ya
uchoraji maarufu Tingatinga kuona shughuli zao na kusikiliza changamoto
mbalimbali wanazokabiliana nazo mapema hii leo 24 Juni 2020 jijini Dar
es Salaam.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam.
24/06/2020
*********************************
Na. WHUSM – Dar es Salaam.
Serikali yawataka Wasanii wa Sanaa ya Uchoraji nchini kujisajili COSOTA
Serikali imewataka wasanii wa
Sanaa ya choraji (Tingatinga) kujisajili katika Chama cha Hakimiliki
Tanzania (COSOTA) ili waweze kunufaika na kazi zao na kuepuka kuibiwa na
kuzulumiwa haki zao kama ilivyo hivi sasa.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
Salaam Wakati Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo,
Juliana Shonza alipowatembelea wasanii hao kwa lengo la kusikiliza
changamoto mbalimbali wanazokutana wasanii hao katika kazi zao.
“Wassanii tumieni fursa hii ya
mabadiliko ya sheria kwa kuhakikisha mnasajili kazi zenu COSOTA ili
muweze kunufaika na kazi zenu vilevile kuepuka kuibiwa na kudhulumiwa
haki zenu,” alisema Naibu Waziri Shonza.
Aidha Naibu Waziri Shonza amesema
kuwa Wizara inaendelea na mchakato wa kuihamisha COSOTA toka Wizara ya
Viwanda na Biashara kuja Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
ambapo hatua iliyofikiwa ni kukamilisha andiko la pamoja kwa ajili ya
kuwasilisha katika mamlaka za uamuzi.
“Tunafanya hivyo ili kuhakikisha
vyombo vinavyoshughulikia haki, maslahi na upatikanaji wa huduma kwa
wasanii vinakuwa chini ya mwamvuli mmoja ili kuwaondolea usumbufu,
gharama na hata upotevu wa stahilli zao,” alisema Naibu Waziri Shonza.
Vilevile Naibu Waziri amewashauri
wasanii hao wafanye kazi zao kwa weledi kwa kuzingatia hali ya
mabadiliko ya teknolojia kwa kutumia njia za mitandao kuuza kazi zao na
kulifikia soko la nje hata katika mazingira magumu kama ya ugonjwa wa
COVID 19 (Corona).
Nae Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha
Ushirika cha Tingatinga Bi. Zena Salum ameiomba serikali ameiomba
serikali kuwatafutia viwanja kwa ajili ya kufanyia shughuli zao kwani
kwa sasa wanachangamoto ya maeneo ya kufanyia kazi zao.
“Tunaiomba serikali itupatie
maeneo ya kufanyia kazi zetu kwani kuna haja ya kupata miundombinu ya
kisasa kwani kwa asilimia tisini wateja wetu ni kutoka nchi za nje,”
alisema Bi. Zena Salum.
Sanaa ya uchoraji imeendelea
kupewa kipaumbele na serikali ikiwa ni pamoja na kuifanyia marekebisho
Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 1999 ili iweze kuendana na
mazingira ya sasa na kumnufaisha msanii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...