Na  Woinde Shizza, KARATU

TAASISI  ya Community Aid and Social Education Empowerment  (CSEE)  kwa kushirikiana  na Child Fund Korea  ambao wamejikita katika kusaidia watoto dhidi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona wametoa msaada wa vifaa venye thamani ya shilingi million 40 kwa Wilaya ya Karatu.

Msaada huo ni vifaa vya kukabiliana na virusi vya corona ambavyo ni  pamoja na  spika za sauti za kusaidia kuelimishia jamii sehemu mbalimbali zenye shughuli zinazokusanya watu wengi kwa  pamoja. 

Akizungumza leo Juni 4,2020, Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo ameshukuru taasisi ya CSEE kwa msaada waliotowa kwa wananchi wa Karatu na kubainisha kuwa  taasisi hiyo  imegusa vijana  wengi hasa kwa kipindi hiki ambacho vyuo na shule za sekondari za kidato cha tano na sita zikiwa zimefunguliwa.

 Amesisitiza msaada umekuja wakati sahihi na  kamati ya wilaya ya Covid-19 itakaa kikao ili kuweka mpangilio mzuri wa ugawaji wa vifaa kwa watoto ma shule.

 Mahongo amebainisha bado anaendelea kutoa elimu kwa watu mbalimbali juu ya namna ya kujikinga na virusi vya corona nakuiomba taasisi hiyo kujikita  katika kambi za wavuvi tarafa ya Eyasi pamoja na sehemu za minada na kutoka elimu katika maeneo hayo 

"Muda mzuri wa kutoa elimu kwenye kambi ni saa 10 jioni ambao ni muda watu wengi wanakuwa wanarudi kwenye mialo  pia nipongeza juhudi zilizochukuliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kukabiliana na covid-19,"amesema Mahongo

Kwa upande wake Ofisa wa Mradi wa CSEE  Ombeni Sakafu amesema taasisi yao  inafanya kazi na watoto na ndio maana wakatoa vifaa ivyo kwa ajili ya kuwalinda ambapo alisema wanategemea  vifaa hivyo vitasambazwa katika shule. 

Ametaja vifaa walivyotoa ni pamoja na  barokoa 500 N95 ,Gun themometre nne za kupima joto ,wamekabidhi box 20 za sabuni za maji ya kunawia mikono, middle’s Paddle hand wash-facilities 35 ,matanki ya kuhifadhia maji kwenye vifaa vya kunawia mikono 20 na  Chlorine powder kilo 126.

Pia Chlorine tablets kilo tano za kuna vitakasa mikono makasha 24, PPE 63, gloves boxes 83, spika 3 kwa ajili ya matangazo ya kuelimisha juu ya corona, vipeperushi 144, vienye ujumbe wa kuelimisha juu ya corona pamoja na bronchure 200 na bango 1na Face shield 333.

Aidha amesema mbali na vifaa hivyo wamejikita katika kutoa elimu kwa njia ya bodaboda ambazo watatumia vipaza sauti kucheza sauti iliyorekodiwa na wataalamu wa afya  juu ya namna ya kujikinga na virusi vya corona. 

Sakafu amebainisha kuwa  watutumia wataalamu wa Halmashauri kutoa elimu ya corona kwa wananchi na watapita kwenye vijiji na magari, kutembelea kaya kuelimisha watu juu ya namna ya kujikinga na Corona.
Theresia Mahongo Mkuu wa wilaya ya Karatu (kushoto) na Katibu tawala  wa wilaya ya Karatu Abbas Kayanda wakikagua vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Corona juzi  vilivyotolewa na   Taasisi ya Community Aid and Social Education Empowerment  (CSEE) ikiwemo spika kwa ajili ya kusaidia kuelisha wananchi wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha (picha na Woinde Shizza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...