Na Amiri
kilagalila,Njombe
Wafugaji wa samaki
mkoani Njombe wametakiwa kuwekeza zaidi katika ufugaji huo kufuatia utafiti
kuonyesha fursa kubwa ya zao hilo kwa aina ya Kambale, Sato na Perege
Kwa muda mrefu
wakazi wa mkoa wa Njombe wamekuwa hawafugi samaki katika baadhi ya maeneo kwa
kuhofia hali ya hewa ya baridi ambapo Niko Msigwa mkulima wa kijiji cha
Kinenulo ameanza kunufaika na ufugaji wa huo
Biashara ya samaki
mkoani Njombe imekuwa na soko la ndani la uhakika na ndio sababu iliyo msukuma
Msigwa kuanza ufugaji huku akikiri kupata faida kubwa.
“Soko la samaki
sasa hivi linafanya vizuri yaani sasa hivi samaki aina ya Sato ni bei
kubwa,ukienda hata sokoni pale kilo moja ni Sh.12,000 na wao wanajumua kilo
moja Sh.7,000 mpaka 8,000”alisema Msigwa
Baadhi ya wakazi wa
kijiji cha Kinenulo wamezungumzia ufugaji na mahitaji ya samaki mkoani Njombe.
“Nilichojifunza
mimi samaki wanafaa kwa matumizi ya binadamu lakini wanaongeza kipato,na
wangejitokeza wengi kufuga ingekuwa vizuri kwasababu hata sisi hapa samaki
wengi wanatoka Njombe”alisema Ephrahim Fungo mkazi wa Kinenulo
Samaki Ambao wapo
Kwenye Kundi Muhimu la Mlo Kamili Kwa ajili ya Lishe Pia Wamekuwa Kitoweo
Kizuri Kwa Watanzania Hatua Inayochagiza Jamii Kuona Umuhimu wa Kuwafuga
Kibiashara.
Ufugaji wa Samaki
ni neema Njombe
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...