Na Emmanuel J. Shilatu
Napenda
niungane na Mamilioni ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
Watanzania kwa ujumla kumpongeza Mwenyekiti CCM Taifa na Rais wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuandika historia ya aina yake kwenye
mkutano Mkuu wa CCM Taifa uliofanyika leo Julai 11, 2020 mjini Dodoma.
Kwanza,
Dkt. Magufuli amethibitishwa kwa kupigwa kura ya ndio na Wajumbe 1822
wote sawa na asilimia 100 kupeperusha bendera ya CCM kugombea urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu
utakaofanyika mwezi Oktoba, 2020.
Haijawahi
kutokea katika historia ya miaka yote ndani ya CCM Mgombea kwa nafasi
ya Urais kupitishwa kwa asilimia 100. Mwaka 2015 Dkt. Magufuli
alipitishwa kwa asilimia 87. Ongezeko hili ni ishara ya kubaliko la
uadilifu, uzalendo, ufuatiliaji, uchapa kazi, ukweli na ucha Mungu
alionao Dk. Magufuli kiuongozi.
Pili,
Dk. Magufuli akiwa Mwenyekiti wa Kikao amewadhihirishia Watanzania na
Dunia kwa ujumla juu ya Demokrasia iliyokomaa, uwazi na Uhuru wa
uchaguzi ndani ya CCM kwa kura kupigwa wazi wazi na kuhesabiwa wazi wazi
tena ikionyeshwa mubashara (live) na vyombo vya habari. Hii rekodi
ameivunja na haijawahi kutokea katika historia ya Miaka yote ya chaguzi
za CCM kwenye nafasi ya kumpata Mgombea Urais.
Hakika,
Dk. Magufuli alivyosema uchaguzi wa mwaka huu atahakikisha unakuwa wa
huru na haki alimaanisha na anaonyesha kivitendo kuanzia ndani nyumbani
kwake (CCM).
Narudia tena
kusema historia aliyoiandika Dkt. Magufuli ni ya aina yake
inayompambanua kivitendo kuwa Mwamba na mkufunzi wa Dunia juu ya siasa
safi, Demokrasia ya kweli na Uhuru wa uchaguzi.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki CCM
Mungu Mbariki Dk. Magufuli
*Shilatu E.J*
0767488622
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...