Naibu waziri wa Kilimo na Mbunge wa Mogorogoro Kusini Mashariki akieleza jambo katika Kata ya KidugaloWajumbe wa Kikao Kata ya Ngerengere wakimsiliza Naibu waziri wa Kilimo juu ya serikali ilivyofanikiwa kuteleza Ilani ya CCM katika kata hiyo.
**************************************


NAIBU waziri wa Kilimo Omary Mgumba amesema kuwa serikali imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali maendeleo kwa wananchi katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki tofauti na watu baadhi ya watu wanavyoeneza propaganda juu ya kile kilichotekelezwa katika jimbo hilo.

Mgumba ambae ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ameyasema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa kamati za siasa katika Kata ya Kidugalo na Ngerengere Mkoani Mkoani Morogoro.

Alisema kuwa wanaoeneza Propaganda hizo hawana nia njema na Chama cha Mapinduzi CCM kwani hivi sasa wananchi wamefunguliwa fursa mbalimbali ikiwemo miundombinu ya Barabara,elimu huduma za afya pamoja na huduma ya maji.

Aidha alisema kuwa hivi sasa wananchi pamoja viongozi wa CCM katika Jimbo hilo wanatakiwa watembee kifua mbele kutokana na yale yalitokelezwa na serikali ya awamu ya tano chini Dr John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yeye akiwa Mbunge wa Jimbo hilo la Morogoro Kusini Mashariki.

Akizungumzia kuhusu Barabara amesema kuwa hivi sasa barabara nyingi zinapitika amabzo zilikuwa changamoto hapo awali hali iliyaofanya wanachi kuteleza shughuli za zao za kimaendeleo licha ya kuwepo changamoto ndogongo katika baadhi ya barabara ambazo serikali imekuwa ikizitatua kwa kwa wakati.

Kuhusu Barabara ya Bigwa Kisaki amesema kuwa barabara hiyo hivi karibuni Itaanza kujengwa kwa Kiwango cha lami kwa Kilometa 60 na makandarasi ameshapatikana hapo awali katika ilani ya CCM 2005 iliahidi kuifanyia upembuzi yanikini ili iweze kujengwa kwa lami

Sanjari na hayo alisema kuwa kwa kipindi cha uongozi wake amefanikiwa kutembelea takribani wa Vijiji na Kata Zote Kila mwaka tofauti na wasikuwa na nia njema wanaodai amekuwa Mbunge wa kata Moja ya Mkuyuni.

ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa jimbo la Morogoro kusini Mashariki kwa ushirikiano wao walioutoa katika kipindi ambacho alikuwa mbunge wa Jimbo hilo

wajumbe hao wa kamati ya Siasa wamempongeza Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Omary Mgumba kwa kufanikwa kuteleza na kutatua changamoto mbalimbali ambazo hapo awali katika viongozi waliopita hazikuweza kutatuliwa.

Walisema kuwa hivi sasa ni faraja kwa serikali awamu ya tano chini Dr John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wanaimani nayo kutokana na miradi mikubwa ya kimkatati ambayo wameitekeleza kwa kipindi kiupi cha miaka miatano.

Waliongeza kuwa juhudi zao katika kusimamia shughuli za maendeleo ndizo zimeifanya sasa serikali hiyo kuingia katika uchumi wa kati.

Jimbo la Morogoro kusini Mashariki chini ya Mbunge wake Omary Mgumba katika kipindi cha awamu ya tano limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupokea fedha za miradi ya maendeleo kupitia mfuko wa Jimbo ambazo zimezaa matunda katika sekta mbalimbali.

Pia wamefanikiwa kudhibiti mapato ya halmsahauri ya Wilaya ya Morogoro ambayo yalikuwa yanapotea mikono mwa wachache,ujenzi wa Kiwanda cha kucahata mazao jamii ya mikunde ambacho ni pekee kwa Tanzania Nzima,pia kujengwa kwa kiwanda Kikubwa cha sukari cha Mkulazi kutafungua fursa kubwa ya ajira kwa wakazi wa jimbo hilo na maeneo mengine.

Ujenzi wa Hospital ya Wilaya,na kuhamishwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mogororo kwenda Mvua yote hayo ni moja ya mafanikio amabyo yamepatikana katika serikali ya awamu ya Tano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...