MKURUGENZI wa Kampuni ya Ushauri wa masuala ya umeme ya (GEARED Consulting Engineers LTD) Mhandisi Ester Ishengoma ameipongeza Serikali ya Awamu ya tano kwa kutoa fursa kwa wahandisi wa ndani na kuwaamini kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati.

Amesema katika kipindi hiki Serikali imetambua uwezo mkubwa walionao wahandisi wa ndani na kutoa fursa ya kuwapa miradi mbalimbali mikubwa kuitekeleza hapa nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi huyo ambaye ni Mtaalamu mshauri wa masuala ya umeme Mhandisi Ishengoma amesema anaipongeza Serikali kwa kuwaamini huku akitolea mfano kampuni yake kupewa mradi mkuwa wa Hospitali ya Kwanga iliyopo Msoma mkoani Mara.

"Wazawa tunapewa fursa tena kubwa katika kipindi hiki hakuna longolongo kwani ukikidhi vigenzo vyao tu unapata kazi bila shaka yeyote .mfano mimi licha ya miradi mingine mingi lakini serikali imeniamini na hivi Sasa kupitia kampuni yangu tunasimamia mradi mkubwa wa ujenzi wa Hospitali ya Kwanga unaoendelea katika eneo la umeme."alisema Mhandisi  Ishengoma.

Kuhusu mradi ambao kampuni yake unaisimamia, Mhandisi Ishengoma amesema atajitajihidi  kuukimbiza na mradi huo ili uweze kukamilika mapema na hatimaye  wananchi wa Mkoa wa Mara na viunga vyake wapate huduma.

Pia amesema licha ya kusimamia miradi mbalimbali hapa nchini lakini pia kampuni yake kutokana na kazi nzuri inazofanya imeweza kuaminika na kupata kazi katika nchi jirani Kama vile Malawi,Zambia na kungineko na hata Visiwani Zanzibar.

Wakati huohuo Mhandisi Ishengoma amesema  moja ya jukumuku la  kampuni yake ni kusanifu Miundombinu ya umeme, na katika kuhakikisha vijana wanasoma masuala ya Ushauri hususani kwenye eneo la umeme wanaiva vizuri na kwamba ameandaa semina ya kuwapiga msasa vijana hao ambao wako vyuoni.

Amesema semina hiyo itafanyika Julau 16 mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa DIT ambapo vijana kutoka vyuo mbalimbali watakutanishwa hapo ili l kupata madini mbalimbali katika sekta ya umeme .

"Semina hii italenga kuwapa ujuzi,na hasa wa kujua mabadiliko ya nyaya za umeme miundombinu mingine kuhusu umeme hivyo semina hii itafanyika Julai 16, 2929 RRale DIT na lengo kubwa nikubadilishana uzoefu na hasa kujua sokoni kuna nini na chuoni kuna nini."amefafanuas Mhandisi Ishengoma.

Hata hivyo amewataka  vijana hao wa kitanzania kuchangamkia fursa hiyo kwani watakuja kupata elimu ya kutosha hususani katika eneo la umeme.


Baadhi ya majengo ya hospitali ya Kwanga ambayo yamo kwenye mradi ambao kampuni hiyo inasimamia
Mkurugenzi wa Kampuni ya Geared Consulting Engineers ltd Estar Ishengoma akizungumzia namna Serikali ya Awamu ya Tano ilivyotoa fursa kwa wahandisi wa ndani kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...