NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametembelea Banda la  Stamico lililopo chini   ya Wizara ya Madini kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Saalaam, leo tarehe 13 Julai, 2020.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutembelea mabanda ya maonesho, amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini imejipanga kuwawezesha wachimbaji wadogo ili wawe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa Sekta ya Madini.

Akielezea mikakati ya Serikali katika kuhakikisha Sekta ya Madini inakua zaidi amesema kuwa ni pamoja na kuhakikisha madini ghafi yanaongezewa thamani nchini kabla ya kusafirishwa nje ya nchi hivyo kuongeza ajira kwa watanzania.

“Kama Serikali tunataka kuhakikisha kuanzia mchimbaji, mchenjuaji, mwongeza thamani hadi mfanyabiashara wa madini ananufaika pamoja na watoa huduma kwenye shughuli za uchimbaji wa madini,” amesema Naibu Waziri Nyongo.

Katika hatua nyingine Nyongo amewataka wachimbaji wa madini kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake.

 Picha ya Pamoja.

NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akipata maelezo mara baada ya kutembelea Banda la  Stamico lililopo chini   ya Wizara ya Madini kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Saalaam, leo tarehe 13 Julai, 2020.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...