Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akionyesha tuzo ya udhamini mkuu wa maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali, katika hafla ya ufungaji rasmi wa maonesho hayo katika Viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam hivi karibuni. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko wa Tanzania, Prof. Riziki Shemdoe.
Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali akikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), kwa kutambua mchango wa NBC katikakudhamini Maonesho  ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yalimalizika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko wa Tanzania Bara, Prof. Riziki Shemdoe.
Mfanyabiashara bilionea  wa Tanzania wa madini ya Tanzanite, Saniniu Laizer (kulia), akipata maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa na NBC alipotembelea katika banda la benki hiyo wakati wa Maonesho  ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (katikati) akipozi kwa picha ya kumbukumbu na baadhi ya maofisa wa benki hiyo katika banda lao wakati wa  Maonesho  ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam hivi karibuni
………………………………………………………………………..
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), imewataka wajasiriamali kutumia huduma bora  za kibenki za NBC ili kunufaika na bidhaa mahususi zinazowalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati ikiwemo mikopo isiyohitaji dhamana.
Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam hivi karibuni na Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru alipokuwa akizungumzia udhamini wao katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar e salaam (DITF), ambapo alisema benki hiyo iliweka nguvu nyingi katika upande wa wafanyabiashara wadogo na wa kati katika kuonesha huduma zao.   
“Benki ya NBC inajivunia mchango wake mkubwa inaoutoa katika kusapoti wafanyabiashara wadogo na wa kati jambo lililoipaisha benki yetu mwaka jana kuwa moja kati ya benki tano  bora barani Afrika katika biashara ya sme’s ikiwa ni moja ya mafanikio makubwa kwa NBC kwa mwaka 2019”, alisema.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa NBC ilishinda tuzo hiyo kutokana na sababu mbalimbali moja ikiwa ni huduma zao wanazozitoa na mikopo ya aina mbaimbali ikiwemo mikopo ambayo haihitaji dhamana kabisa na inayotoka kwa muda mfupi kwa ajili ya wajasiliamali wadogowadogo.
“NBC katika kuonyesha kuwa tunawathamini wafanyabiashara hawa na kutambua umuhimu wa mchango wao katika kuchangia uchumi wa Taifa na pia kuboresha biashara zao ndio maana kwa maonesho ya mwaka huu tumedhamini banda maalumu la wajasiriamali hao tuliowatoa katika ngazi ya chini na sasa wakiwa katika ngazi ya juu ili waoneshe biashara zao”, alisema Bwana Ndunguru.   
Aidha mkurugenzi huyo alisema NBC inatoa pia huduma Huduma ya kuwaongezea uwezo wajasiriamali katika shughuli zao mfano ikiwa ni pamoja na kujifunza utunzaji wa kumbukumbu, namna bora ya ulipaji wa kodi za Mamlaka ya Mapato (TRA) na pia kupanua wigo wa biashara zao kwa safari za kimafunzo nje ya nchi ikiwemo China na nchi nyingine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...