IKIWA ni miaka miwili tu tangu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) uanzishwe, umekuja na mfumo wa kisasa wa kutoa huduma kwa wanachama wake kupitia njia ya mtandao yaani (online portal), Mhandisi wa Mifumo ya kompyuta (System engineer) wa Mfuko huo Eng. Goodluck Msangi amesema.
Akieleza jana jinsi mfumo huo unavyofanya kazi kwenye banda la PSSSF katika maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba, Eng. Msangi alisema mfumo huo unawawezesha wanachama na wastaafu kupata taarifa mbalimbali kuhusu mwenendo wa michango na taarifa za malipo ya pensheni ya kila mwezi.
“Kwa wanachama wanaweza kupata taarifa ya mwenendo wa michango yao iliyowasilishwa na mwajiri, mstaafu ataweza kupata taariza za malipo ya pesnheni ya mwezi kiasi kilicholipwa na benki amayo kiasi hicho cha fedha kimelipwa….. pia  mfumo huo unawezesha mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mwanachama au mstaafu na mfuko wakati wowote na mahala popote bila ya muhusika kuhitajika kufika kwenye ofisi za Mfuko.” Alifafanua Eng. Msangi.
Aidha kupitia mfumo huo endapo mwanachama ana maoni, ushauri au anahitaji ufafanuzi wa jambo lolote anaweza kufanya hivyo na mrejesho akaupata mara moja.
Alisema mfumo huo unapatikana kwenye tovuti ya mfumo yaani www.psssf.go.tz.
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere (aliyekaa kulia), akisaidiwa kuangalia michango yake katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Kaimu Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma PSSSF, Abdul Njaidi (wapili kushoto) na Afisa Matekeleza Mwandamizi wa Mfuko huo, Donald Meeda wakati alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam katika viwanja vya Julius Nyerere maarusu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Julai 5, 2020.
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere (kushoto), akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la PSSSF kwenye maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam katika viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba jijini Dar es Salaam leo Julai 5, 2020. Wanaomuhudumia ni   Kaimu Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (wapili kulia) na Afisa Uhusiano Bw. Meseka Kadala.

 Afisa Matekelezo Mwandamizi PSSSF, Bi. Zainab Ndullah (kushoto), akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo.
 Mwanachama akisubiri huduma katika banda la PSSSF.
  Mwanachama akiangalia hali ya michango yake katika Mfuko.
Bw. Meeda (kushoto) akimuelekeza mtiririko wa michango mwanachama huyu aliyetembelea banda la PSSSF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...