Na Said Mwishehe, Mchuzi TV

RIDHIWANI kikwete amerudisha fomu ya kuomba ridhaa katika chama chake CCM, kuwania ubunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika octoba 25, 2020.

Amerejesha fomu hiyo leo julai 16, mwaka huu katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi "CCM" mkoani humo, ambapo amesema baada ya kukamilisha hatua hiyo ya kurejesha fomu anasubili taratibu nyingine ambazo zimewekwa na chama chake.

Hata hivyo alipoulizwa kama anachochote cha kueleza, Ridhiwani amejibu kwamba ratiba ya chama chake hiko wazi kuwa kuanzia julai 14 hadi julai 17 ni wakati wa kuchukua na kurejesha fomu, hivyo mengine atazungumza wakati ukifika.

Pamoja na hayo amesema "   kubwa zaidi naomba ushirikiano kama ilivyokuwa miaka mitano iliyopita nikiwa mbunge wa Chalinze".




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...