Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Serikali imetoa sh.bilioni 40 ajili ya ukarabati na ujenzi wa vyuo vipya 25 vilivyojengwa katika Halmashauri tatu nchini.

Hayo ameyasema Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) Peter Sitta  katika maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya sabasaba amesema  tayari wilaya  waandishi wa habari jana katika maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya sabasaba  amesema tayari wilaya tatu zimeshakamilisha ujenzi huo ambao ni Nkasi, Kasulu na Ileje.

Amesema ,kwa mwaka wa fedha ulioisha kulikuwa na miradi ya ujenzi na upanuzi wa vyuo 40.Sitta amesema lengo lao ni kuongeza udahili kutoka  704,000 hadi 1,000,000 kufikia mwaka 2020.

Hata hivyo Sitta amesema,lengo lao ni kuona wanafunzi wakiwa wabunifu wa kubuni vitu mbalimbali na kuweza kutatua changamoto za wananchi.

,Tunatambua maendeleo ya viwanda yanahitaji ujuzi na ubunifu ili kuwe na viwanda bora na vinavyozalisha bidhaa zinazotumika kwa wananchi kwa VETA kuwa suluhisho "amesema Sitta

Vilevile alisema, katika maonyesho hayo ya 44 wameleta teknolojia mpya 12 ambazo ni,kuzidua unga wa ubuyu,kuchemsha maji pasipotumia umeme,kuingiza umeme kwenye mita,ushonaji,kupanda mazao,ukaushaji wa samaki na teknolojia ya kuchenjua madini  kutoka kwenye makenikia bila ya kutumia zebaki ambayo tayari imeshapigwa marufuku.
 Mwanafunzi wa Chuo cha VETA Chang'ombe Dafrosa Anthony Akitoa maelezo jinsi wanavyotengeneza vitakasa mikono ambavyo ni tahadhari ya kujikinga na virusi vya Corona vilivyopo katika maonesho ya Sabasaba.
 Mtaalam wa VETA Dodoma Reagan Swai akizungumza  kuhusiana taratibu zinazotakiwa kufuatwa katika uandaji wa nyama kutoka mfugo hadi kuwa nyama.
 Wananchi wakipata maelezo ya alama za usalama barabarani wakati walipotembelea Banda la VETA maonesho ya biashara kimataifa sabasaba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...