SERIKALI imesema hadi kufikia Agosti mwaka huu italipa fidia ya Sh Bilioni 16 kwa wakandarasi wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko katika Jiji la Dodoma ili kukwepa adhabu na fidia kadiri ya mkataba walioingia na wakandarasi hao ya kuimarisha na kubadilisha mandhari ya Jiji la Dodoma na kulifanya kuwa na sura na hadhi ya kimataifa  .

Hayo yamesemwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe  wakati wa hafla ya utiliaji  saini wa mradi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara za mzunguko katika Jiji la Dodoma.

Amesema kama serikali haitotimiza masharti hayo ya mkataba italazimika kulipa pesa pamoja na adhabu na hivyo kuchelewesha mradi kutokamilika kwa wakati,

“ Kwa hiyo sasa fidia hizi zipo na zitalipwa kwa mujibu wa sheria, Wakuu wa Wilaya nao wapo ,kamati za ulinzi na usalama nazo zipo ,na wala sio vikundi vya ajabu ajabu vinavyojitokeza kuwa wao ndio wanaofatilia fidia ,serikali iko makini na itatekeleza hilo kwa wakati.”Amesema

Aidha amemtaka Mkurugenzi wa Jiji La Dodoma kuhakikisha anapima na kugawa viwanja bure kwa wawekezaji waweze  kuharakisha upatikanaji wa huduma za kijamii  katika maeneo ya mradi huko ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa ajira kwa makundi mbalimbali wakiwemo vijana ,akina mama na watu wenye ulemavu.

“Na mimi nikushauri Mkurugenzi  pima viwanja bure ,wewe unaweka tu mahesabu yako vizuri na watakapojenga wewe unaanza kuirudisha ile hela kwa kukata kodi yako ,na usipofanya hivyo utatengeneza hali ya ucheleweshaji katika maeneo hayo,na wewe mwenyewe umeshaona umeoona unapima eneo unasema milioni nane atanunua nani.”Amesisitiza Waziri Kamwelwe.

Kwa upande wake mtendaji mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale amesema katika kuhakikisha mradi huo wa ujenzi wa barabara unakamilika kwa wakati Benki ya maendeleo ya Africa imetoa mkopo wenye masharti nafuu wa  kiasi cha shilingi bilioni 412 na serikali inachangia shilingi bilioni 82,ikiwa ni asilimia 16.5 ya gharama yote ya ujenzi huo .

“ Na barabara hii imegawanywa katika maeneo mawili na sehemu ya kwanza ni kutoka nala ,veyula ,mtumba hadi ihumwa kwenye bandari kavu nyenye kilomita 52.5, na sehemu ya pili ni kutoka ihumwa bandari kavu ,matumbulu hadi bandari kavu hadi nala tena,na barabara hii itajengwa kwa njia nne.”Amesema Mfugale.

Naye mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr Binilith Mahenge amesema mafaniko haya ya Jiji la Dodoma Kupata Miradi ya kimakati ni matokea ya Serikali kuhamishiwa Dodoma na Dodoma kuwa Jiji na kwamba ujenzi wa Barabara hizo utabadilisha madhari ya Jiji na  kulifanya kuwa Jiji La kibiashara litakalohimili ushindani katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii ,ikiwemo elimu na sekta ya afya.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe akishuhudia utiliaji saini kati ya mkandarasi wa mradi huo na Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Patrick Mfugale leo jijini Dodoma.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza katika hafla ya utiliaji saini wa barabara ya mzunguko jijini Dodoma leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge akizungumza katika hafla ya utiliaji saini mikataba ya barabara ya mzunguko jijini Dodoma leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...