Baadhi ya watumishi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala wakati akifungua mafunzo ya kimataifa ya kukabiliana na Covid-19 pamoja na magonjwa ya mlipuko ikiwa ni mkakati wa kuwandaa watumishi hao kupokea wageni mbalimbali wa kimataifa wanaoingia nchini Tanzania.
Balozi wa Ujeruman nchini Tanzania Regine Hess(aliyesimama) akizungumza sababu za ubalozi huo kufadhili mafunzo ya kimataifa ya kukabiliana na Covid-19 kwa watumishi wa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA).Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Julai 13,2020 na Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala.
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Paul Rwegasha(aliyesimama) akieleza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kimataifa ya kukabiliana na Covid-19 ambayo yametolewa kwa watumishi wa uwanja huo ambao ndio wanaohusika na kupokea wageni kutoka nchi mbalimbali duniani wanaoingia nchini kwa usafiri wa anga.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Uchumi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Daniel Malanga akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya kimataifa ya namna ya kukabiliana na Corona.

Wakufunzi walioandaliwa kwa ajili ya kutoa mafunzo ya kimataifa yanayohusu kukabiliana na magonjwa ya  mlipuko ukiwemo wa Covid-19 wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo ambayo yamefunguliwa rasmi na Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala(katikati) akiwa na Balozi wa Ujeruman nchini Tanzania Regine Hess, maofisa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere pamoja na baadhi ya watumishi wa uwanja huo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzinduliwa rasmi kwa mafunzo hayo.
Sehemu ya watumishi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii.Dk.Hamis Kigwangala wakati akifungua mafunzo ya kimataifa ya kukabiliana na Covid-19.Mafunzo ya siku nne yameanza leo Julai 13,2020 na yamefadhiliwa na Ubalozi wa Ujeruman nchini Tanzania.
Balozi wa Ujeruman nchini Tanzania Regine Hess akifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala (hayupo pichani) baada ya kuzindua mafunzo ya kimataifa ya kukabiliana na Corona. 




Baadhi ya watumishi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala wakati akifungua mafunzo ya kimataifa ya kukabiliana na Covid-19 pamoja na magonjwa ya mlipuko ikiwa ni mkakati wa kuwandaa watumishi hao kupokea wageni mbalimbali wa kimataifa wanaoingia nchini Tanzania.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala(aliyekaa katikati) akiwa pamoja na Balozi wa Ujeruman nchini Tanzania Regine Hess (aliyekaa wa kwanza kushoto) wakifuatilia kikao cha ufunguzi wa mafunzo ya kimataifa ya kukabiliana na Covid-19 yaliyoandaliwa kwa watumishi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.










Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MAFUNZO ya kimataifa ya kukabiliana na ugonjwa wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam huku Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangala akisisitiza umuhimu wa watumishi wa viwanja vya ndege nchini kuendelea kuchukua hatua zote zinazopaswa kuchukuliwa kukabiliana na ugonjwa huo.

Akizungumza leo Julai 13,2020 wakati akifungua mafunzo hayo ya kimataifa kwa watumishi hao, Dk.Kigwangala amefafanua mafunzo hayo ni muendelezo wa kuendelea kuchukua tahadhari kwa wageni wanaokuja nchini na iwapo itabainika kuna mgonjwa mwenye dalili za Covid-19 iwe rahisi kupata huduma na wakati huo huo kuwakinga wengine.

Kwa mujibu wa Dk.Kigwangala mafunzo hayo yamefadhiliwa na Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania na yanaviwango vyote vya kimataifa katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko likiwemo janga la Covid-19 hasa kwa kuzingatia magonjwa hayo yataendelea kutokea duniani, hivyo kuna wajibu wa kujiandaa katka kuyakabili.





Amefafanua Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto iliandaa muongozo katika kukabiliana na Covid-19 na miongoni mwa maelekezo ni kuandaliwa kwa mafunzo ya aina hiyo kwa ajili ya watoa huduma walioko kwenye sekta ya utalii ikiwemo wanaopokea wageni na wale ambao wanawahudumia watakapokuwa nchini.

"Kama mnavyofahamu mashirika mengi ya ndege ya kimataifa yametoa taarifa za kuanza safari za ndege tena, hivyo tumeamua kuwandaa watu wetu.Mafunzo haya yana kiwango cha kimataifa kama ambavyo imeshauriwa na Shirika la Afya Duniani(WHO) katika kuendelea kupambana na Covid-19.

"Tunataka wageni wanapokuja nchini kwetu wawe na uhakika na afya zao , hivyo tutawahudumia kulingana na maelekezo mbalimbali ya kimataifa.Sisi kama nchi tumejipanga kikamilifu tunataka wageni wanapokuja waone namna ambavyo tunachukua tahadhari zote kulingana na maelekezo ya kimataifa.Hatutaki watoke hapa na kwenda kuichafua nchi yetu.

"Hivyo ni matarajio yetu wanaopata mafunzo hayo watazingatia yale yote ambayo watafundishwa na wakufunzi wetu.Ni kweli chini ya Rais wetu mpendwa Dk.John Magufuli tumefanikiwa kukabiliana na Corona na sasa tunaendelea na maisha yetu kama kawaida lakini kwa wageni wanaokuja lazima tuendelee kuonesha hatua tunazochukua kukabiliana na Corona,"amesema.

Hata hivyo amesema tayari mafunzo hayo yameshafanyika kwa kada nyingine zilizopo katika sekta ya utalii wakiwemo watoa huduma katika hoteli za kitalii, waongoza watalii pamoja na madereva na sasa yanayotolewa kwa watumishi wa viwanja vya ndege.Zanzibar tayari yamefanyika na baada ya hapo yatatolewa kwa watumishi wa Uwanjwa wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro(KIA).

Hata hivyo amefafanua kutokana na umuhimu wa mafunzo hayo, ndio maana ubalozi wa Ujeruman nchini Tanzania umeona haja ya kuyafadhili ili kuhakikisha yanatolewa katika kiwango cha kimataifa.

Kwa upande wake Balozi wa Ujeruman nchini Tanzania Regine Hess amesema nchi yao inatambua jitihada zilizofanywa na Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na Corona lakini ipo haja ya kuendelea kutolewa mafunzo ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ambayo yanaweza kutokea wakati wowote kama ilivyo kwa Covid-19.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Paul Rwegasha pamoja na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Uchumi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Daniel Malanga wameeleza kwamba mafunzo hayo ni muhimu na wanaamini tayawaongeza maarifa zaidi ya kukabiliana na kuchukua hatua zaidi ya kujikinga na ugonjwa huo katika maeneo ya viwanja vya ndege.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...