Na Janeth Raphael,Michuzi TV.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Amina Salim Ali amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Dk John Magufuli pamoja na Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kwa jitihada walizochukua kukabiliana na janga la Covid-19 ambao linaisumbua dunia kwa sasa.

Amesema kwamba Tanzania imekua nchi ya mfano kwa majirani zake na Ulaya kwa ujumla kwa namna ambavyo maraisi wetu walivyojitoa  mhanga kwa kukataa kufungia wananchi wake ndani na kutoa uhuru wa kuendelea na shughuli za kila siku za kujitafutia kipato kwa ajili yao na familia zao.
Balozi Amina Salim Ali ameyasema hayo leo Julai 13, 2020 wakati akifunga Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yaliyokua yanaendelea yanafanyika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

"Viongozi wetu wakuu, Rais Dk.Magufuli pamoja na Rais Dk.Shein wanastahili kila aina ya pongezi katika kukabiliana na janga la Corona.Pia tunampongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake ambazo zimetuweza nchi yetu kuingia katika uchumi wa Kati. Hakika hii ni hatua kubwa Sana ambayo Tanzania tuimepiga na kutuwezesha kuingia katika nchi zinazoendelea, tunajivunia kwa hilo,"amesema Balozi Amina.

Kuhusu maonesho hayo ya biashara ya kimataifa, amewapongeza TANTRED kwa kufanikisha maonesho hayo ambayo yamefana kwa kiwango kikubwa ingawa nchi bado imegubikwa na taharuki ya ugonjwa wa Covid-19."TANTRAD lazima tuwapongeze kwa kufanikisha maonesho haya, tangu mwanzo hadi leo hii tunapoyahitimisha."

WAZIRI wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Amina Salim Ali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...