Na.Vero Ignatus.

Mikakati inayotumika katika kuhakikisha ajali za pikipiki zinapungua kupungua, ni pamoja na usimamizi na udhibiti kwa watoaji na watumiaji ,utoaji wa elimu kwa kutumia vyombo vya habari kama radio, televisheni na magazeti, kuandaa vipeperushi vya elimu kwa waendesha pikipiki, kutoa mafunzo katika vituo (vijiwe) mbalimbali vya waendesha pikipiki. 

Mratibu wa Elimu kwa umma PC Rajabu kutoka jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Arusha, anasema kuwa ajali za pikipiki (bila idadi)kwamba kipindi cha mwaka 2019-2020 Januari- Augusti kwa mkoa wa Arusha ,zimepungua kwa kiasi kubwa, kutokana kwamba wamejikita zaidi katika suala nla utoaji wa elimu ya masuala ya usalama barabarani katika makundi yote ya watumiaji wa barabara hususani waendesha pikipiki

Tumekuwa tukiwafuata katika vituo vyao wanapopaki bodaboda ,kwa kupitia vyuo vya udereva kwa kuwahamasisha kwenda kusoma, ili waweze kuona tofauti na kuzifahamu sheria kanuni za usalama barabarani, japokuwa changamoto bado zipo, katika baadhi ya maeneo kutokana na Jiografia ya mkoa wa Arusha ilivyo 

Anasema changamoto bado zipo ikiwemo maeneo yasiyofikika kirahisi kutokana na uharibifu wa miundombinu ila wamekuwa wakijitahidi kiwafikia kwaajili ua kuwapatia elimu usalama barabarani ili kufikia lengo hku akisema ni jukumu la kila mmoja kuwasaidia asiyoweza kuvuka barabara na siyo kwa jeshi la polisi pekee. 

Faustin Matina ni mkuu wa chuo cha Wide Instute of Diving kilichopo Moshi -Kilimanjaro anasema katika mpango wa kupunguza ajali za barabarani Tanzania ,wamekuwa wakishirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani ambapo wamefanikiwa kuifikia mikoa yote Tanzania Bara ,katika utoaji wa elimu kwa madereva wa pikipiki waliosajiliwa katika vijiwe vyao. 

''Kabla ya kuanza kutoa mafunzo haya kwa kushirikiana na Jeshi la polisi ajali pikipiki barabarani ,zilikuwa ni nyingi sana ,kwakweli vijana walikuwa wanakufa ,kwasababu walikuwa hawajui matumizi sahihi ya barabara na haswa umuhimu wa kuvaa kofia ngumu''Anasema

Baada ya mafunzo kwa sasa ajali zimepungua,kwa sababu ya elimu inayotolewa mara kwa mara,anasema kwamba ajali zinakuwepo kwasababu bodaboda ni zao la kila siku, na baadhi yao wanatumia ukaidi wa kutokutii , kutokufuata sheria na kanuni za usalama barabarani 

Baadhi ya madereva pikipiki hawavai kofia ngumu,abiria haswa wakina mama hawavai kutokana na sababu mbalimbali, ni kweli hazizuii ajali bali zinapunguza madhara haswa kichwani inapokuwa imetokea ajali ya barabarani.

'' Katika kuwafikia makundi yanayotumia barabara hususani waendesha bodaboda kwa utafiti mdogo walioufanya bodabioda ndiyo miongoni mwa watumia barabara kwa kutenda makosa barabarani na hata kusababisha ajali zinazopelekea vifo na majeruhi na uharibifu wa mali mbalimbali ''

Kwa upandwe wake dereva bodaboda anayefahamika kwa jina la Tumaini Kimaro amekiri kupewa elimu marakwamara juu ya matumizi sahihi ya barabara ,na kusema kuwa ajali sivyo kama ilivyokuwa awali kabla ya kupatiwa elimu hiyo

Watembea kwa miguu nao wanatakiwa wapatiwe elimu ya kutosha juu kwenye alama za pundamilia kwani wengine wanakuwa bize na simu hawavuki kwa wakati au mwingine wanakuwa na msongo wa mawazo unaowasababisha hata kusahau kuwa wapo barabarani jambo ambalo linaweza kuwasababishia ajali wakati wowote ule.

''Kwavile inamruhusu kuvuka basi anakuwa kama anafanya kusudi unakuta yupo bize na kuchati au anaendelea na mtandao bila kujali yupo barabarani,pia anasema wengine sijui ni msongo wa mawazo ama ninini wanajisahau kama wapo barabarani ''alisema 

Akizungumza mwananchi Juma Idi anasema usafiri huo wa pikipiki, unasaidia kupunguza kwa kasi kubwa tatizo la usafiri katika maeneo mengi nchini 'haswa maeneo ambayo usafiri wa magari hauna uhakika na hayawezi kufika, wananchi wa kipato cha chini wanaweza kutoka eneo moja kwenda lingine kwa gharama nafuu.

Ameongeza kuwa kwasasa walau akiwa anatumia usafiri huo akimwambia dereva wa pikipiki atembee mwendo wa kawaida ,anamuelewa tofauti na ilivyokuwa awali, madereva hao walikuwa wanatumia kauli zisizo sahihi kwa wateja wao

''Inaonekana jeshi la polisi limefanya kazi ya ziada kwa madereva hawa hata ajali hatuzisikii kama ilivyokuwa mwanzoni jamani,hata kwa usafi wamekuwa wasafi ni baadhi tu amabao hawataki wameamua kuwa wachafu''alisema

Kauli ya serikali iliyosomwa Bungeni kuhusu ajali zinazotokana na matumizi ya pikipiki nchini kwa mujibu wa takwimu za jeshi la polisi nchini katika kipindi cha kuanzia januari 2012- mei 2013 idadi za pikipiki zilizosajiliwa nchi nzima ilikuwa 10,036 mikoa inayoongoza kwa wingi wa pikipiki ni Jiji la Dar es salaam,lenye jumla ya pikipiki 4,434,wilaya ya Kinondoni pekee ina jumla ya pikipiki 1,735,Temeke 1,363,Ilala 1,334,mikoa inayofuata kwa idadi kubwa ya pikipiki ni Morogoro 811,Arusha 644 na kilimanjaro 479.

Katika kipindi cha januari hadi disemba 2012 kulitokea jumla ya ajali 5,763ambazo ziligharimu maisha ya watanzania 930 na kujeruhi wengine 5,532,katika mkoa wa dar es salaam uliongoza kwa kuwa na ajali 2,479 ambapo wilaya ya kinondoni nilikuwa na ajali 1,007,Temeke 769 na Ilala 703 amabapo ajali hizo zilisababisha vifo 164 na majeruhi 2,745 ambapo idadi hiyo ilikuwa kubwa,Arusha 509,vifo 65 na majeruhi 420,Morogoro ajali 431 vifo 54 majeruhi 328,mkoa wa Kilimanjaro ajali 294 vifo 52 na majeruhi 266.

Katika kipindi cha Januari -Mei 2013, takwimu zinaonyesha kuwa kumetokea ajali za pikipiki 2,415 nchi nzima ambapo ajali hizo zimesababisha watu 352 kupoteza maisha na wengine 2,368 kujeruhiwa, 

Mkoa wa Dar es Salaam umeongoza kwa matukio ya ajali 2,161 zilizosababisha vifo 56 na majeruhi 1,210 kwa mchanganuo ufuatao:-Wilaya ya Kinondoni ajali 515, vifo 22 na majeruhi 549, Temeke ajali 299, vifo 19 na majeruhi 354 na Ilala ajali 357, vifo 15 na majeruhi 307. 

Takwimu za Mikoa mingine iliyoongoza kwa wingi wa ajali ni Mkoa wa Morogoro uliokuwa na ajali 186 zilizosababisha vifo 15 na majeruhi 117, Arusha ajali 118, vifo 16 na majeruhi 102, Kilimanjaro ajali 130, vifo 26 na majeruhi 120, mkoa wa Pwani ajali 114, zilizosababisha vifo 23 na majeruhi 167. 

Matukio ya ajali za pikipiki ni mengi kwa mujibu wa takwimu nilizozitaja hapo juu, idadi ya vifo na majeruhi ni kubwa kiasi cha kusababisha hospitali nyingi nchini kuanzisha wodi maalum za majeruhi wa pikipiki,hatua za makusudi zisipochukuliwa,Taifa litaendelea kuathirika na ajali hizi ambazo zinachukua maisha ya watu wengi na kuongeza idadi ya yatima, walemavu na watu wasiojiweza na kuwafanya wawe tegemezi.

vyanzo vikuu vya ajali za barabarani zinazohusisha pikipiki ni pamoja na kutokujua Sheria, Kanuni na taratibu za matumizi ya barabara ambapo madereva wengi wa pikipiki hawana leseni za udereva, uendeshaji wa hatari wa pikipiki barabarani kwa kwenda mwendo wa kasi na kupita magari mengine bila sababu, kupita katika taa za kuongozea magari (traffic lights) bila kuruhusiwa, kudharau askari wa usalama barabarani wanaoongoza magari katika makutano ya barabara, kupakiza abiria watatu au zaidi katika pikipiki maarufu kama mshikaki na matumizi ya vilevi. 

Sababu nyingine ni miundombinu ya barabara ambapo baadhi ya barabara zinakosa alama, au zinakuwa na alama zilizofifia ambazo si rahisi kuonekana, barabara kutumika na makundi yote ya watumiaji (traffic mix) ambapo magari, pikipiki, baiskeli, mikokoteni (maguta) na watembea kwa miguu pamoja na ubovu wa barabara (mashimo na matuta). Madereva wa magari kutoheshimu wapanda pikipiki ni sababu nyingine kubwa inayosababisha ajali za pikipiki nchini. 

Madereva wa magari mara nyingi wamekuwa hawatoi ushirikiano mzuri kwa madereva wa pikipiki wanapokuwa barabarani, tabia hiyo ya madereva wa magari inatokana na mtazamo hasi, kuhusu waendesha pikipiki, ambapo watu wengi wanaamini kuwa waendesha pikipiki hawana nidhamu barabarani.

Mikakati mbalimbali inafanywa na Jeshi la Polisi katika kukabiliana na wimbi kubwa la ajali za pikipiki ili kunusuru hali hiyo ambapo Mafunzo haya yanafanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama Asasi Zisizo za Kiserikali na vyuo vya udereva hususan VETA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...