Na Said Mwisheh,Michuzi TV

MAKATIBU Wakuu wa Wizara ya Katiba na Sheria kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) pamoja na maofisa waandamizi wa wizara hizo wamekutana jijini Dar es Salam kwa ajili ya kujadiliana masuala ya itifaki mbalimbali ikiwemo za ajira, kazi na takwimu.

Wametumia nafasi hiyo pia kuelezea masuala ya kisheria pamoja na changamoto zake ikiwa ni mpango mkakati wa kutafuta ufumbuzi wake katika jumuiya hiyo huku ikifafanuliwa kuwa bado katika nchi hizo kuna changamoto ya mlolongo katika upitishaji wa sheria za pamoja na zile za kimataifa kwasababu kwa sasa karibu kila nchi imekuwa na utaratibu wake katika masuala ya kisheria.

Akizungumza leo Agosti 3,2020 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na  Sheria nchini Tanzania Profesa Sifuni Mchome ambaye ndio Mwenyekiti wa mkutano huo amesema kikao hicho kimehusisha maofisa mbalimbali waandamizi ,wanasheria pamoja na  maakatibu wakuu wa wizara ya Katiba na Sheria katika nchi za jumuiya hiyo.

 "Kupitia mkutano wa leo pamoja na mambo mengine tutapa fursa ya kujadili kasoro zilizopo katika masuala ya kisheria na kisha kuzitafutia ufumbuzi wake .Moja ya lengo ni kurahisisha  upitishwaji wa itifaki na sheria mbalimbali katika ukanda wetu wa jumuiya ya nchi za SADC,"amesema.

Profesa Mchome ameongeza zipo baadhi ya itifaki ambazo hazijatiliwa mkazo katika jumuiya hiyo ,miongoni mwa itifaki hizo ni inayohusu uuzajwi silaha pamoja na udhibiti wa silaha ndogo ndogo ambazo zimekuwa zikiingizwa kinyume na sheria."Kutokana na hali hiyo wameona haja ya kuweka itifaki katika kudhibiti suala hilo la silaha."

Kupitia kikao hicho ,Katibu Mkuu ameweka wazi kuwa makatibu wakuu hao pamoja na maofisa wa ngazi mbalimbali wataweka mipango ya kushughulikia mambo kadhaa yakiwemo ya hali ya ulinzi na usalama huku pia wakijadiliana kuhusu kukabiliana na matukio ya uhalifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...