Na Khadija Seif, Michuzi TV

KATI ya wasichana 10 wanaofanya vizuri katika anga ya Muziki wa kizazi kipya alias bongofleva , huwezi kuacha kumtaja mwanadada Nandy.

Nandy ambae kwa Sasa amepata dili nyinyi na kuonekana miongoni mwa wasichana wenye maendeleo.

Nandy ambae kwa sasa ni balozi wa makampuni mengi likiwemo  kampuni ya nywele aina Darling amesema pamoja na kipato chake lakini sio mtu wa majivuno na kujiona super star.

Nandy akizungumza na Michuzi TV wakati wa kutambulisha bidhaa mpya ya nywele ya darling amesema anapenda maisha ya kujichanganya na watu tofauti tofauti  ili ajifunze vingi.

"Mara nyingi nimekua mtu wa kula na mashabiki kwenye sehemu mbalimbali ila huwa sio mtu wa kujionyesha Sana kiasi watu wanashindwa kujua Kama huwa ni moja ya vitu ambavo napenda,"

Hata hivyo wakati huo huo nandy aliwanunulia mashabiki zake mishikaki ya shilingi elfu 25 na kuwagaia ikiwa ni sehemu ya kuonyesha kuwa anayapenda maisha ya kula pamoja na shabiki zake 

pia nandy amekanusha kuwa na ugomvi na Lulu diva.

"Ni maneno tu wala msiyafuatishe, Mimi ni shabiki wa Luludiva na Mara nyingi nasikiliza wimbo wake wa Gugugaga,"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...