WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameitaka mikoa yote nchini kuwa na mkakati wa kutoa takwimu za hali ya lishe Kila baada ya miezi mitatu.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo jijini Dodoma katika maadhimisho ya siku ya lishe kitaifa yenye kauli mbiu "Mlo kamili kwenye jamii yetu inawezekana" .

Amesema lengo la maadhimisho hayo ni kutathmini hali ya lishe nchini ambapo amesema kukiwa na lishe bora maradhi hayatakuwepo.

Kuhusu hali ya udumavu hapa nchini Waziri Ummy amebainisha kuwa kwa tafiti za mwaka 2018 udumavu umepungua kutoka asilimia 34.4 mwaka 2014 hadi asilimia 31.8 mwaka 2018 .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya chakula na lishe Tanzania(TFNC) Dkt. Germana Leyna amesema udumavu kwa watoto  Tanzania upo chini ya asilimia 30,Unene asilimia 30,upungufu was damu kwa wajawazito asilimia 30 na Unene wastani wa asilimia 30.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye siku ya Lishe duniani ambayo imefanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya chakula na lishe Tanzania(TFNC) Dkt. Germana Leyna akizungumza katika siku ya Lishe leo jijini Dodoma.
Wanafunzi wa Lishe kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma waliojitokeza kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma katika siku ya Lishe duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...