Na Woinde Shizza , michuzi Tv Arusha
WANANCHI wametakiwa kunywa maziwa kwa wingi pamoja na kuwapa watoto wao  kwani maziwa yanasaidia vitu mbalimbali mwilini ikiwemo kuongeza akili kwa watoto na kuwa na kumbukumbu za kutosha.

Hayo yalisemwa jana na Meneja masoko wa kampuni ya kusindika na kutengeneza maziwa  (the Grande Demam's)Jacob Nyosole wakati akiongea na waandishi wa habari  Katika kilele cha maonyesho ya 27 ya nanenane kwa kanda ya kaskazini  yaliofanyika Katika viwanja vya Themi vilivyoko njiro Ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha mkoani hapa.

Alisema kuwa maziwa yanasaidia Mambo mengi mwilini ikiwa Ni pamoja na kuboresha afya ya mwili , kutengeneza miili yenye afya ,maziwa yanatengeneza uchangamfu kwa watoto pamoja na kumjenga mtoto kuwa na afya njema

Aidha alisema kuwa, changamoto kubwa iliyopo ni kwa wananchi wengi kutokuwa na mwamko wa kutosha Katika kunywa maziwa, hivyo elimu zaidi inatakiwa kutolewa ili wananchi waendelee kunywa maziwa kwa wingi .

Alifafanua zaidi kuwa, wamekuwa na soko Katika maeneo mbalimbali kutokana na ubora wao walio nao, hivyo aliwataka wananchi kuhakikisha wanatumia kwa wingi maziwa  kutoka kiwanda hicho ili kuboresha afya zao.

Nyosole alitumia fursa hiyo kuwataka wafugaji kuhakikisha wanafuga kisasa zaidi  kwa kutumia ushauri wa wataalamu ili waweza kupata malighafi zilizo bora zaidi na kutoa maziwa yaliyobora .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...