Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya Kuzuia na Kupambana biashara haramu ya usafirishaji wa bianadamu, Adatus Magere akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kufungua Kongamano linalojadili na kutathimini mikakati ya Serikali dhidi ya biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu, ambalo limeshirikisha wadau mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali na Binafsi.

Mkuu wa Mradi wa kupambana na Biashara haramu ya Binadamu kutoka shirika la IOM, David Hofmeijer akichangia mada katika Kongamano linalojadili na kutathimini mikakati ya Serikali dhidi ya biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu, ambalo limeshirikisha wadau mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali na Binafsi.
 Mkuu wa Mradi wa kupambana na Biashara haramu ya Binadamu kutoka shirika la IOM, David Hofmeijer akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika Kongamano linalojadili na kutathimini mikakati ya Serikali dhidi ya biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu, ambalo limeshirikisha wadau mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali na Binafsi.




 Picha za Pamoja.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
IKIWA siku ya Kimataifa ya kupambana na biashara haramu ya binadamu hufanyika kila mwaka ifikapo Julai 30, hapa nchini watu 61 wakuhumiwa kwa kosa la kufanya biashara haramu binadamu, watu 12 kesi zao zikiendelea katika mahakama mbalimbali hapa nchini huku wahanga 557 waokolewa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, mara baada ya kufungua Kongamano linalojadili na kutathimini mikakati ya Serikali dhidi ya biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu, ambalo limeshirikisha wadau mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali na Binafsi, Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya Kuzuia na Kupambana biashara haramu ya usafirishaji wa bianadamu, Adatus Magere amesema kuwa tatizo la usafirishaji haramu wa binadamu ni kubwa kwani biashara hiyo hufanyika kwa usiri Mkubwa.

Magele amesema kuwa usafirishaji haramu wa bianadamu unashika nafasi ya tatu katika makosa makubwa ya kimataifa ikiongozwa na biashara haramu ya siraha na biashara ya Dawa za kulevya.

"Watu wanaofanya biashara hii haramu imekuwa vigumu sana kuwapata mpaka vyombo vya sheria vinapowagundua na takwimu hazionekani katika uhalisia." Amesema Magere.

Hata hivyo Magere amesema kuwa Kuendelea kwa Changamoto ya uwepo wa biashara haramu ya binadamu katika Kamati ya Kuzuia na Kupambana biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu ni ufinyu wa bajeti inayosababisha wasiwafikie wahanga wa biashara hiyo haramu.

Licha ya hilo Magere amasema kuwa  uelewa wa jamii na mtu mmoja mmoja nao unachangia kuendelea kuwepo kwa biashara haramu ya binadamu kuchanganya na uhamiaji haramu wa binadamu.

"Watu wengi wanaichanganya tatizo la usafirishaji haramu wa binadamu na wahamiaji haramu kama ambao wamekuwa wakipitishwa hapa nchini kupelekwa Afrika Kusini, matatizo haya ni mawili tofauti, la kwanza ni kusafirishwa kwa huiari yao 'Uhamiaji haramu', na biashara haramu ya binadamu kwa anayesafirishwa anakuwa hajui malengo ya msafirishaji." Amesema Magere.

Kwa upande wake Katibu wa Sekretarieti ya Taifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu,  Separatus Fella amesema kuwa kutokana na tafiti mbalimbali zinazofanyika kimataifa zinaonesha kuwa tatizo la usafirishaji haramu wa binadamu zipo.

"Takwimu za 2016 hadi 2020 zinaonesha kuwa watu waliohukumiwa ni 61, kesi 12 zinaendelea katika Mahakama mbalimbali na wahanga wa biashara haramu ya binadamu hapa nchini ni 557..." Amesema Fella.

Hata hivyo Fella amebainisha kuwa changamoto kubwa ya kuendelea kuwepo kwa biashara haramu ya binadamu ni umasikini katika jamii kwani familia nyingi zinapokea fedha kidogo kwa kudanganywa na kutoa mtoto kwenda kufanya kazi mahali bila kujua kama ni kosa.


Nae Mkuu wa Mradi wa kupambana na Biashara haramu ya Binadamu, David Hofmeijer amesema kuwa biashara haramu ya binadamu ni sawa na biashara mpya ya utumwa inayoendelea kimya kimya licha ya kuwepo na taasisi za kimataifa na kitaifa za kupambana na biashara haramu ya binadamu.

Amesema kuwa wanashirikiana na Wizara ya Mambo ya ndani, Shirika la IOM na UN  ili kuhakikisha biashara haramu ya bianadamu inakomeshwa hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...