Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akizinduwa rasmi huduma maalum ya kuhakiki pembejeo inayofahamika kwa jina la 'T-hakiki' ndani ya Banda la Shirika la Mawasiliani Tanzania (TTCL), kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayofanyika viwanja vya Nyakabindi Mkoa wa Simiyu. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Patrick (kushoto) Ngwediagi wakishiriki tukio hilo.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Patrick Ngwediagi (kushoto) wakipiga makofi mara baada ya uzinduzi huo.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma maalum ya kuhakiki pembejeo inayofahamika kwa jina la 'T-hakiki' ndani ya Banda la Shirika la Mawasiliani Tanzania (TTCL), kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayofanyika viwanja vya Nyakabindi Mkoa wa Simiyu. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba.
Wageni waalikwa katika tukio hilo wakishuhudia uzinduzi.
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba akizungumza kwenye uzinduzi huo wa huduma maalum ya kuhakiki pembejeo inayofahamika kwa jina la 'T-Hakiki', ulofanyika ndani ya Banda la Shirika la Mawasiliani Tanzania (TTCL), kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayofanyika viwanja vya Nyakabindi Mkoa wa Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akipongezana na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba mara baada ya tukio hilo.


Na Mwandishi Wetu, Simiyu
WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga leo amezinduwa rasmi huduma maalum ya kuhakiki pembejeo inayofahamika kwa jina la 'T-hakiki'. Waziri Hasunga amezinduwa huduma hiyo, leo ndani ya Banda la Shirika la Mawasiliani Tanzania (TTCL), kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayofanyika viwanja vya Nyakabindi Mkoa wa Simiyu.

Alisema huduma hiyo imetokana na ubunifu wa Shirika la Mawasiliani Tanzania (TTCL), Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu Ukanda wa Tropiki (TPRI/TAPHPA), wakilenga kumkomboa mkulima.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu Ukanda wa Tropiki (TPRI), Dk. Margaret Mollel amesema ubunifu huo umeenda sambamba na malengo ya Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo.

"..Uuzaji wa pembejeo bandia za kilimo una athari kubwa kiuchumi na kijamii. Athari hizo mbali na kuathiri sekta ya kilimo pia uathiri kiasi kikubwa cha maendeleo ya wakulima nchini. Kwa sasa huduma hii itamsaidia mkulima kufahamu matumizi sahihi ya pembejeo hizo kupitia simu ya mkononi, hakika haya ni mapinduzi bora ambayo yatazidi kumkomboa mkulima lakini pia kuisaidia Serikali kukabiliana na wafanyabiashara wa pembejeo wasio waadilifu...," alisema Dk. Mollel.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba akizungumza katika uzinduzi huo, alisema mbegu na viuatilifu feki kwa wakulima imekuwa changamoto kubwa ambayo imeathiri pia ukuaji wa sekta ya kilimo.

Aliongeza kuwa,  TTCL imeliona hilo na kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu Ukanda wa Tropiki wamekuja na suluhisho.

"...T-Hakiki itaboresha sekta ya kilimo na italinda maisha ya wakulima wengi katika kuendesha shughuli za kilimo na kulinda thamani ya fedha zao," alisema Kindamba.

Alisema; "..T-Hakiki ni mfumo wa njia ya SMS ambapo mkulima atatakiwa kubofya *148*52# na kuingiza namba ya siri iliyopo kwenye vifungashio vya mbegu, mbolea au kwenye chupa za vifungashio vya mbegu, mbolea au kwenye chupa za viuatilifu ili kuthibitisha uhalisi wa pembejeo,"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...