Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega (kushoto) akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi na Wananchi leo Kata ya  Nyamato.(Picha na Emmanuel Massaka michuzi Tv)
Mwanachama mpya wakipokea Kadi za CCM.

 MGOMBEA katika nafasi ya ubunge mh Abdallah Ulega*anaendelea na ziara yake ya kampeni katika Jimbo la mkuranga ambapo Jana alikuwa katika kijiji cha *mkonoge kata ya Nyamato.

Mgombea huyo ambaye amewawakilisha vyema wananchi wa Jimbo la mkuranga katika kipindi cha miaka mitano ya serikali ya Chama cha mapinduzi ameendelea kuwaomba wananchi wa Jimbo hilo kuendelea kuiamini serikali yao na kuhakikisha wanakipa Ushindi wa kishindo chama cha mapinduzi ili kiendelee kushika Dola.

 Mgombea huyo wa ubunge jimbo la Mkuranga ndg Abdallah Ulega aliwaeleza wananchi hao wa kijiji cha Mkanoge Kata ya Nyamato juu ya mambo makubwa  yaliyofanyika katika mwaka wa 2015-2020 ambapo serikali ya ccm imefanikiwa kujenga Zahanati ya kijiji na tayari inatumika na kupatikana kwa nishati ya umeme wa uhakika ambapo wananchi wanaendelea kufurahia huduma hiyo,

Mh Abdallah Ulega amewaomba wananchi hao wampe ridhaa ya kuwatumikia tena Kwa kipindi cha miaka mkutano na kuhakikisha wanampa Kura za kutosha Rais Magufuli ili waweze kuendelea kuwaletea maendeleo wananchi wa kata ya Nyamato na vijiji vyake, Pia mh *Ulega aliwaeleza wananchi hao waliofurika Kwa wingi  kuwa katika miaka mitano ijayo ameahidi,

Kuimarisha miundombinu ya barabara.

Kusambaza huduma ya umeme zaidi Ujenzi wa shule shikizi kwenye kitongoji cha Kisaraka na kadhalika.

Vile vile mgombea huyo amewataka wananchi siku ya tarehe 28 October wanajitokeza Kwa wingi kwenda kupiga Kura na kuhakikisha wanachagua  viongozi wote wa ccm ya Rais, Mbunge na Diwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...