MSANII Rutyfiya Abubakary maarufu kama 'Amber Rutty' na mpenzi wake Said Bakary pamoja na mwenzao James Charles 'James Delicious' wamehukumiwa kulipa faini ya sh. Milioni 11 ama kutumikia kifungo cha miaka mitano  jela baada ya kupatikana na hatia katika makosa matatu likiwemo kosa la  kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Hata hivyo washtakiwa hao, wameshindwa kulipa faini hiyo na hivyo wamepelekwa gerezani.

Hukumu hiyo imesomwa leo Septemba 25, na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambaye amesema, mahakama imewatia hatiani washtakiwa wote baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi kumi wa upande wa mashtaka ambao wameweza kuthibitisha makosa pasipo kuacha shaka yoyote.

"Nimezingatia hoja zilizotolewa na pande zote mbili na athari za makosa haya, ni kweli washitakiwa wote ni vijana na wanategemewa, nimeona mshitakiwa wa kwanza anajutia, washtakiwa wote watatu ni wakosaji wa mara ya kwanza, kutokana na mazingira ya kesi hii adhabu yake ni miaka 30 kila kosa ambapo nikiwafunga mtapotea kabisa..., hivyo kwa mazingira mliyoyasema na lengo la adhabu ni kujirudi, mshitakiwa wa kwanza utalipa faini ya sh. milioni tatu ama jela miaka mitano,  mshitakiwa wa pili utalipa faini ya milioni tatu ama jela miaka mitano na mshitakiwa wa tatu utalipa faini ya sh. milioni tano ama jela miaka mitano. Amesema Hakimu Isaya.

Kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo,  Hakimu Isaya aliuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusoma ndipo Wakili wa Serikali, Faraja Nguka alieleza "Hakuna rekodi za makosa ya nyuma za washtakiwa, 

"Mheshimiwa, makosa waliyotiwa nayo hatiani washtakiwa ni makosa ambayo yamezuiliwa hata na vitabu vitukufu na yana  madhara makubwa kwa jamii na hayana tiba,  tunaomba mahakama iwape adhabu stahiki ili iwe fundisho kwao na kwa wengine wenye nia ya kutenda makosa kama haya", amesema Ngukah

Katika utetezi wao, Amberutty amesema aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ana watoto wanamtegemea, mmoja ana matatizo ya Pumu, pia na wazazi wake wanamtegemea yeye na kwamba , ana maradhi ya T.B yanamsumbua,

Mshtakiwa Bakary aliiomba mahakaka isimpe adhabu kali kwani yeye ni mtoto mkubwa anayetegemewa na familia ya watoto watatu na mama ni mzee pia anasumbuliwa na TB na anatumia vidonge.

Kwa upande wake, mshitakiwa James kupitia Wakili wake alisema "Naomba mahakama itoe adhabu ndogo kwa sababu hajawahi kutiwa hatiani wala rekodi ya jinai. Pia alionyesha ushirikiano tangu shauri lilipofunguliwa Mahakamani. Pia ni mtu aliyeonyesha utii na wito uliotolewa na RC aliutii na kufika Polisi. Pia mshitakiwa ni kijana mwenye umri mdogo familia yake inamtegemea, na ana mzazi mmoja".

Akichambua hukumu hiyo, Hakimu Isaya amesema katika hukumu hiyo kulikuwa na hoja saba ikiwemo kama mshitakiwa Amberutty ndiye aliyeonekana katika video ya ngono ama lah, pia kama mshitakiwa huyo ameingiliwa kinyume na maumbile ama lah, pia kama mshitakiwa Said alimuingilia kinyume Amberutty .

Hakimu Isaya amesema kuwa baadhi ya hoja hazikuwa na shaka ikiwemo iliyomuhusu mshitakiwa Amberutty ambaye alipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kufanyiwa vipimo sehemu ya nyuma na kubaini kupo wazi.

Katika kesi hiyo kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile lilikuwa linamkabili Amber Rutty, ambapo anadaiwa kati ama baada ya October 25, 2018 alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya October 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile.

Aidha katika kosa la kuchapisha video ama picha za ngono mitandaoni inadaiwa kati ya October 25,2018 James Deliciouw alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...